Aomba talaka kisa mume wake haogi

Aomba talaka kisa mume wake haogi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mwanamke mmoja nchini India amewaacha watu vinywa wazi baada ya kuomba talaka kwa mumewe ikiwa ni siku siku 40 tu baada ya harusi yake, akidai kuwa mume wake hapendi kuoga na hawezi kuendelea kukaa naye

Mwanamke huyo alifikisha malalamiko yake kwenye kituo cha ushauri nasaha cha familia cha Agra nchini humo na kueleza kuwa mumewe ambaye alimtaja kwa jina moja la Rajesh anaoga mara moja au mbili tu kwa mwezi.

Kituo hicho kilifanya jitihada za kumuita mwanaume huyo na alikiri kuwa ana tatizo hilo kweli na malalamiko ya mke wake ni ya kweli na kukiri kuwa tangu waoane ameoga mara sita pekee

Kufuatia mazungumzo ya muda mrefu Rajesh alikubali kuwa atabadilisha tabia hiyo na kuanza kuoga kila siku

Pamoja na hayo mkewe amekataa kuendelea kuishi naye ambapo wanandoa hao wameagizwa kurejea katika kituo cha ushauri nasaha Septemba 22 kwa ajili ya masuluhisho zaidi
 
Kuna jamaa miaka ya 1988,tukiwa form 2huko Mbeya, wilaya ya Rungwe, alikuwa haogi wiki nzima siku akioga watu wa bwenini wote mtajua tuu,atajisifu balaa kwamba mwanaume lazima upige povu mwilini!Si povu Hilo la sabuni!
 
Back
Top Bottom