Apan Cheza na Middle Income Kwenye Maswala ya Teknolojia

Tony254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2017
Posts
16,017
Reaction score
16,431

Kama huna bundle ya kutosha kaa kando wenzako watatazama video na kukuhadithia.
 
ongereni majirani tuko njiani
Karibu ndugu yangu. Sisi huku mwanafunzi anapoingia shuleni, anatia kidole chake kwenye kidude kisha kidude hicho kinatuma ujumbe kwa simu ya mzazi kuwa mwanawe amewasili shuleni. Wakati wa mwanafunzi kurejea nyumbani ukifika, vilevile mwanafunzi anatia kidole kwenye hicho kidude kisha hicho kidude kinatuma ujumbe kwenye simu ya mzazi kuwa mwanawe ametoka shuleni. Hii itazuia mambo mengi ikiwemo wanafunzi wanaokosa kuripoti shuleni na kuenda kupiga maraundi mwenda mjini, au wanafunzi wanaotoka shuleni na kuchelewa kuwasili nyumbani hawatakuwa na sababu nzuri ya kumdanganya mzazi kwani mzazi tayari anajua wakati mwanawe alipotoka shuleni. Utundu,anasa,kujivinjari, kupiga maraundi, team kadinya na tabia zingine zitapungua. Shule mia moja zinatumia hiki kidude Nairobi.
 
Tanzania huku tunatumia Serikalini, Kama ni mfanyakazi wa Serikali ukiingia unaweka kidole ina scan fingerprint na inapiga picha hapo hapo, lakini sijajua Kama ni ofisi zote hadi za chini
 
Hii noma kwa kweli ingeletwa enzi zetu sijui ningefanya nini maana nilikua napenda kukwepa kwepa darasa. Hongera ndugu zangu Wakenya, tuhakikishe watoto wetu wanapata elimu na wanabaki shuleni muda wote maana hawa ndio Kenya ya kesho.
 
Tanzania huku tunatumia Serikalini, Kama ni mfanyakazi wa Serikali ukiingia unaweka kidole ina scan fingerprint na inapiga picha hapo hapo, lakini sijajua Kama ni ofisi zote hadi za chini
Kenya tumeintroduce kwa shule zetu pia
 
Tanzania huku tunatumia Serikalini, Kama ni mfanyakazi wa Serikali ukiingia unaweka kidole ina scan fingerprint na inapiga picha hapo hapo, lakini sijajua Kama ni ofisi zote hadi za chini

Tatizo wanawake wenu wanapenda kutumia hena sana kwenye vidole, nimewahi kufanya installation ya biomtric system kwenu ilikua mtihani sana kwa wanawake, ilitulazimu kutumia facial recognition kwa wale wa hivyo.
 
Unagusa king'amuzi HALAFU unasepa zako kitaa badala ya klasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…