Apatikane Mbadala wa DAWASA na TANESCO ili kuongeza ushindani na ufanisi wa utoaji huduma

Apatikane Mbadala wa DAWASA na TANESCO ili kuongeza ushindani na ufanisi wa utoaji huduma

Tengeneza Njia

Senior Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
121
Reaction score
205
Wadau,

Katika kipindi chote cha kuona serikali tofauti tofauti hapa Tanzania kero ambazo zimekuwa zikijirudia rudia sana ni hii ya upatikanaji wa maji na umeme.

Watanzania wameshazoea kuiomba serikali kupewa huduma hizi kitu ambacho ni haki yao tena ya msingi kama walipa kodi.

Ifike mahali tutumie historia kama best practice kuona namna ambavyo tunaweza kujikwamua katika changamoto ambazo imekuwa kama trend kuendelea kutokea na changamoto hizi kutumika na wanasiasa kujinadi wanapotaka kupewa kura vipindi vya uchaguzi kuwa "mkinichagua nitawaletea maji, umeme etc."

Tulitokaje kwenye mfumo wa kuwa na kampuni moja tu ya mawasiliano (ya kiserikali TTCL) mpaka sasa ambapo yapo makampuni mengi na wananchi wanapata nafasi ya kuchagua huduma ya simu wanaotaka.

Ifike sasa sekta binafsi iruhusiwe kuanzisha mifumo mingine itakayokuwa inatoa huduma za maji na umeme kubwa zaidi tofauti na kutegemea hizi za serikali tu, kama tulivyokuwa na mashirika ya bima tofautitofauti.
 
huwezi pata izo huduma uku unalalamika nyuma ya keyboard.... tukiingia barabaran mapema tu heshima itapatikna
 
Back
Top Bottom