Apoteza maisha kwa kuudhiwa na mke

Apoteza maisha kwa kuudhiwa na mke

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
54,762
Reaction score
59,204
Mwingine huyu hapa! Apoteza maisha kwa kuudhiwa na mke
5528542.jpg

Thursday, March 17, 2011 10:57 AM
MKAZI wa Mbezi Juu Mtoni jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la Shabani Kihundo (30), amekutwa amekufa akiwa chumbani kwa kuhisiwa kunywa sumu kwa kuudhiwa na mkewe katika ujumbe aliouacha chini ya kitanda. Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Bw. Charles Kenyela alisema kuwa, Kihundo alikutwa amekufa juzi chumbani kwake majira ya saa 7 mchana akiwa amelala kifudifudi.

Kamanda Kenyela alidai kuwa, Kihundo aliacha ujumbe uliooneshwa kuwa kulikuwa na ugomvi kati yake na mkewe ujumbe aliokutwa chini ya kitanda chake.

Kamanda Kenyela alifafanua kuwa ujumbe huo ulisomeka hivi: “Nimejiua kutokana na kutoelewana na mke wangu, nimeona nimuachie dunia name niondoke duniani nikatulize nafsi yangu japokuwa nilimpenda”

“Nimekuachia hiyo nyumba,japo kuwa ulininyima haki yangu, mimi ni mwanachama wa NSSF na kadi yangu anayo mke wangu,

“Yeye apewe milioni moja ili ziweze kumsaidia kwa sababu atakuwa na maisha magumu, nimeahca baiskeli apewe mdogo wake mke wangu pamoja, nguo na viatu”

“Pia Samweli ananidai shilingi 28,000 asante”ulimaliza ujumbe huo

Maiti imechukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
 
Mwingine huyu hapa! Apoteza maisha kwa kuudhiwa na mke
5528542.jpg

Thursday, March 17, 2011 10:57 AM
MKAZI wa Mbezi Juu Mtoni jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la Shabani Kihundo (30), amekutwa amekufa akiwa chumbani kwa kuhisiwa kunywa sumu kwa kuudhiwa na mkewe katika ujumbe aliouacha chini ya kitanda. Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Bw. Charles Kenyela alisema kuwa, Kihundo alikutwa amekufa juzi chumbani kwake majira ya saa 7 mchana akiwa amelala kifudifudi.

Kamanda Kenyela alidai kuwa, Kihundo aliacha ujumbe uliooneshwa kuwa kulikuwa na ugomvi kati yake na mkewe ujumbe aliokutwa chini ya kitanda chake.

Kamanda Kenyela alifafanua kuwa ujumbe huo ulisomeka hivi: "Nimejiua kutokana na kutoelewana na mke wangu, nimeona nimuachie dunia name niondoke duniani nikatulize nafsi yangu japokuwa nilimpenda"

"Nimekuachia hiyo nyumba,japo kuwa ulininyima haki yangu, mimi ni mwanachama wa NSSF na kadi yangu anayo mke wangu,

"Yeye apewe milioni moja ili ziweze kumsaidia kwa sababu atakuwa na maisha magumu, nimeahca baiskeli apewe mdogo wake mke wangu pamoja, nguo na viatu"

"Pia Samweli ananidai shilingi 28,000 asante"ulimaliza ujumbe huo

Maiti imechukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.

Huyu atakuwa mhehe tu!
 
Back
Top Bottom