Apple iMac huwa zinafaa kwa shughuli za stationary?

Apple iMac huwa zinafaa kwa shughuli za stationary?

sheby blogger

Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
23
Reaction score
22
Wadau naomba msaada kidgo kujua kama,

Kompyuta za apple znaweza kufaa kutumika katika kazi za stationary bila kuleta matatizo au usumbufu wowote? Maana nlitaka kununua kuna jamaa yangu akaniambia mizigo ya apple huwa ni utumwa au wenyewe wanaita ni gereza la kifahari.

Nikaona sio mbaya nije kuomba ushauri huku kabla nisije kujichanganya.
 
1. Tofautisha Stationary na Stationery

2. Zinafaa lakini issue ni payback period ( unless hujazinunua).

3. Nunua machine ambazo baada ya miezi 10 umerudisha gharama za vifaa vyote. then unaanza ku generate faida na kupambana Kodi ya pango (na ya kijana wa kazi if employed)
 
Wadau naomba msaada kidgo kujua kama, kompyuta za apple znaweza kufaa kutumika katika kazi za stationary bila kuleta matatizo au usumbufu wowote? Maana nlitaka kununua kuna jamaa yangu akaniambia mizigo ya apple huwa ni utumwa au wenyewe wanaita ni gereza la kifahari, nikaona sio mbaya nije kuomba ushauri huku kabla nisije kujichanganya.
Hapo stationery mnataka kuitumia kwa kazi gani?
 
Swali zuri, hata mimi mda tuu nilikua natamani kupata jibu, Wadau nao naona badala watoe Majibu ya inafaa au haifai technically, wanasuguria kunguni
 
Yeyote anaesema Apple ni gereza na Ufahari, yeye ndio yuko katika Gereza za Fikra
 
Mkuu kuna sababu kwanini windows ipo sana Maofisini.

Mac itafanya kazi ikiwa unajua kila kitu unachonunua na kazi zipo kwenye Mpangilio, ila ukiweka Mac kisha ukaenda kwenye mtumba kuchagua printer tegemea matatizo kuanza, Mac haina legacy support kama windows.

Windows yenyewe inaSupport almost vitu vyote toka ianzishwe, unaweza ukaweka printer hata yenye drivers za win Xp, ngumu kukuta vifaa vya kiofisi havifanyi kazi kwenye windows.
 
Mkuu naona unapenda ufahari kwenye utafutaji wa pesa,Mimi ofisini kwangu natumia dell na hp na huu Ni mwaka wa nne sasa sijaona tatizo,nakushauri utumie dell na HP achana na mbwembwe zako,dell na HP zangu nilinunua kwa sh 300,000 tu kwa kila computer
 
Mac ni expensive alafu compartibility na vifaa vingine ni shida kidogo. yaani hapo labda uweke Mac compartible devices tupuu which is very expensive!
 
Hizo mashine ni zetu sie DJs zinatumika kurun lile DJ program korofi la Serato DJ Pro huwa linatulia sana kwenye hizi mashine na hata video mix zinakua vizuri hakuna lagging, kulitumia kwenye windows tunalazimikaga kutafuta gaming PC..

Wewe tafuta windows computer kwa ajili ya kazi zako hizo za ofisi ya stationery, mbona zipo nyingi tu na bei ni affordable..
 
Garama yake iko juu, na sio user friendly..yaani itachukua muda kumfundisha atakae tumia! Pia kama wengine walivyosema ikija mambo ya printing kuelewana na printer ni mpaka udownload drivers!
 
Wadau naomba msaada kidgo kujua kama,

Kompyuta za apple znaweza kufaa kutumika katika kazi za stationary bila kuleta matatizo au usumbufu wowote? Maana nlitaka kununua kuna jamaa yangu akaniambia mizigo ya apple huwa ni utumwa au wenyewe wanaita ni gereza la kifahari.

Nikaona sio mbaya nije kuomba ushauri huku kabla nisije kujichanganya.
Mkuu tafuta HP,Dell achana na apple Imac. sitaisahau ilichonifanyia
 
Haxifaa hata kidogo kutokana apple kuwa na limit option kuna baadhi ya kazi za wateja utashindwa kuzifanya ,pia uwekezaji km huo utahidi umpate mtu ambaye anabasic kubwa ya knowldge ya kompyuta maana apple zina ugumu katika matumizi

sent from HUAWEI
 
Nina ka steshenari kangu na nina tumia iMac

Kazi kubwa ya iMac kwenye kasteshenari kangu ni kuandika na kuprint

Nimeiunga na printer na scanner

Sijawahi kupata shida yoyote tajwa hapo juu zaidi ya changamoto ya matumizi pale unapopata mfanyakazi mpya.

Wengi hawawezi kutumia iMac

Inabidi umpe darasa kidogo la namna ya kutumia
 
Back
Top Bottom