BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Apple Inc leo Jumatatu imesema itatengeneza toleo la simu za iPhone 14 nchini India, ikiwa ni mpango wake wa kuhamisha baadhi ya teknolojia za uzalishaji wa vifaa vya kamouni hiyo kutoka China.
Kampuni hiyo ilizindua simu kuu ya iPhone 14 katika hafla ya mapema mwezi huu, ambapo iliangazia uboreshaji wa usalama badala ya uainishaji mpya wa kiufundi.
"Msururu mpya wa iPhone 14 unaleta teknolojia mpya za msingi na uwezo muhimu wa usalama. Tunafurahi kuwa tunatengeneza iPhone 14 nchini India," Apple ilisema katika taarifa.