Apps za mikopo za mtandaoni zinakopesha kwa riba kubwa sana

Apps za mikopo za mtandaoni zinakopesha kwa riba kubwa sana

Joined
Jul 26, 2022
Posts
10
Reaction score
19
Hizi Apps za online loan zimekuwa kero zinakopesha pesa ndogo Kwa riba kubwa ukichelewa kuwalipa unaongezewa penalty kubwa sana.

Yaani imekuwa changamoto maoni yangu kwa serikali wazicontrol vizuri zinaumiza sana ikiwezekana zifutwe tu.
 
Utajuaje kama zimesajili maana Hawa majama usipowalipa ni wasumbufu kinoma Everytime wanatuma message kugipa simu ndio usiseme
 
Hizi apps za online loan zimekuwa kero zinakopesha pesa ndogo Kwa riba kubwa ukichelewa kuwalipa unaongezewa penalty kubwa sana yaani imekuwa changamoto maoni yangu Kwa serikali wazicontrol vizuri zinaumiza sana ikiwezekana zifutwe tu[emoji441][emoji441]
Njia sahihi ya kuzifuta ni USIKOPE. Wewe na mwenzako na rafiki yako na ndugu yako. Hakikisha hakuna anayekopa, zitajifia au zitashusha gharama za kukopa.
 
Hawa tusipokopa. Kama mwezi wote wanafunga. Mtu ana mtaji wa mil 10 tu anaanzisha kampuni ya kukopa.
 
Hawa jamaa sio poa, kuna siku nikajichanganya nikasema ngoja nione kama kweli wanakopesha,nikajaza kila kitu wakanambia naweza kopa 56,000. Wakaleta terms and conditions,ile kuaccept haikupita dakika muamala ukasoma.

Kuangalia wamenipa 35k...yan zaidi ya 20k ni riba!

Niliwalipa muda huo huo na app nikaifuta maana sikuwa na shida na ile hela. Sasa nimelipa wananiambia naweza kopa 100k, kama kwenye 56k walikata 20k kwenye hiyo 100k si watachukua 40k nzima?

Kifupi usijaribu kukopa kwa hawa jamaa, na nasikia usipolipa wanaanza kutuma sms kwenye contracts zako.

Kifupi jamaa ni wapigaji, mwenye kusikia na asikie!
 
Yaani hawafai ni wanyonyaji mno riba zao ni 100% hawa na hata muda haujafika wanaanza kukupigia simu na kuwatumia sms watu uliowasave kwenye phone book yako kiufupi BOT ingeanza kuwatazama hizi app za mitandaoni ni zaidi ya kausha damu
 
Wanawajuaje hao watu wako waliopo katika phone book yako?

Siku moja nimekaa natafakari maisha yanavyonipeleka puta, mara meseji ikaingia katika simu "HABARI NDUGU AMA JAMAA WAKARIBU WA XYZ MWENYE NAMBA YA SIMU ABCD NI TAPELI AMEKOPA KIASI CHA SHILLINGI 79860/= KUTOKA KAMPUNI YA EFGH NA ANATAKA KUTUTAPELI, UKIWA KAMA MTU WAKE WA KARIBU TUNAOMBA UMUAMBIE ALIPE DENI LAKE KABLA HATUJAANZA KUCHUKUA HATUA NYINGINE JUU YAKE.

Huyo jamaa namfahamu. Baada ya kupata meseji hiyo ikabidi niwapigie kuwauliza, namba yangu wamepata wapi? Wakasema wamejipata kwa njia zao wenyewe. Nikampigia jamaa (anayeitwa tapeli) akasema, ni kweli alikopa, ila namba yangu hakuwapa.

Hadi sasa najiuliza, namba katika phone book, wanapataje?
 
Ukifanya installation ya app, kuna option ya kukubali access ya contacts, sms, location nk. Ukitoa access ndio wanachukua file lote la contacts zako. Apps nyingi zina huo upuuzi, nadhani wana violate haki za mteja.
 
Back
Top Bottom