Aminoltetranguloxide
Member
- Jul 26, 2022
- 10
- 19
Njia sahihi ya kuzifuta ni USIKOPE. Wewe na mwenzako na rafiki yako na ndugu yako. Hakikisha hakuna anayekopa, zitajifia au zitashusha gharama za kukopa.Hizi apps za online loan zimekuwa kero zinakopesha pesa ndogo Kwa riba kubwa ukichelewa kuwalipa unaongezewa penalty kubwa sana yaani imekuwa changamoto maoni yangu Kwa serikali wazicontrol vizuri zinaumiza sana ikiwezekana zifutwe tu[emoji441][emoji441]
Huwa huwalipi? Ukikopa lipa boss. Soma masharti, fahamu gharama za mkopo, kopa kisha lipa ndani ya muda au acha USIKOPE.Utajuaje kama zimesajili maana Hawa majama usipowalipa ni wasumbufu kinoma Everytime wanatuma message kugipa simu ndio usiseme
Wanawajuaje hao watu wako waliopo katika phone book yako?Yaani hawafai ni wanyonyaji mno riba zao ni 100% hawa na hata muda haujafika wanaanza kukupigia simu na kuwatumia sms watu uliowasave kwenye phone book yako kiufupi BOT ingeanza kuwatazama hizi app za mitandaoni ni zaidi ya kausha damu
Ukifanya installation ya app, kuna option ya kukubali access ya contacts, sms, location nk. Ukitoa access ndio wanachukua file lote la contacts zako. Apps nyingi zina huo upuuzi, nadhani wana violate haki za mteja.Wanawajuaje hao watu wako waliopo katika phone book yako?
Siku moja nimekaa natafakari maisha yanavyonipeleka puta, mara meseji ikaingia katika simu "HABARI NDUGU AMA JAMAA WAKARIBU WA XYZ MWENYE NAMBA YA SIMU ABCD NI TAPELI AMEKOPA KIASI CHA SHILLINGI 79860/= KUTOKA KAMPUNI YA EFGH NA ANATAKA KUTUTAPELI, UKIWA KAMA MTU WAKE WA KARIBU TUNAOMBA UMUAMBIE ALIPE DENI LAKE KABLA HATUJAANZA KUCHUKUA HATUA NYINGINE JUU YAKE.
Huyo jamaa namfahamu. Baada ya kupata meseji hiyo ikabidi niwapigie kuwauliza, namba yangu wamepata wapi? Wakasema wamejipata kwa njia zao wenyewe. Nikampigia jamaa (anayeitwa tapeli) akasema, ni kweli alikopa, ila namba yangu hakuwapa.
Hadi sasa najiuliza, namba katika phone book, wanapataje?