mcndomba maprosoo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2013
- 225
- 94
Umaskini na uharibifu wa mazingira ni watoto pacha na mama yao ni ujinga, (A.H Mwinyi, 2010). Nimelazimika kuanza na usemi huo wa Mzee Ruksa nikiikumbuka kila April 1, ambapo huwa ni siku ya wajinga (foolish day) sina uhakika kama wajinga wenyewe wanaumoja na uongozi uliothabiti. Kwani wanapatikana wapi? Nani ni muasisi wa chama hiki?
Lengo na madhumuni yake ni nini? Vision na misheni je? Nani wadhamini wa kundi hili? Kitaifa imefanyika wapi? Nini kauli mbiu ya mwaka huu? Mgeni rasmi alikuwa nani? Vyombo vya habari wamemnukuu nani katika yale waliyo ya ripoti? Kwa nini sherehe hizi ziishie saa 4.00 asb tu?,Kwa nini ikawa April 1?
Kumbe katika wale maadui watatu ujinga, umaskini na maradhi bosi wao ni ujinga? ndiyo maana akaja kuwa mama yao? Ooh! Ndiyo. Mbona hata katika yale matatu ya mtume Paulo upendo ndiyo bosi wao, Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu ; na katika hayo lililo kuu ni upendo, (1Kor 13:13). Kwa nini hatukuhangaika na moja kwanza?
Tunawezaje kuwakusanya wajinga wanaozungumzwa hapa ili tuone mikakati ya kuuondoa? Tuungane pamoja na Sulemani mwana wa Daudi katika kuelimisha ili kuutokomeza ujinga badala ya kuushabikia, mkamate sana elimu usimwache aende zake; mshike maana yeye ni uzima wako,( Mith 4:13). Kila mmoja aguswe na hili. Pamoja tunaweza!