binafsi simjui aliyeianzisha
nafikiri wanasaidia kidogo kufurahisha manake utakuta ujinga mwingie hadi mtu anatabasamu. naona baadhi ya post zinatoa changamoto ya watu kutafakri kabla ya kukubali kitu. nindhani kuwa kuwtokana na uangalifu unaochukuliwa katika habari siku hii ya wajinga inawezekana ndiyo siku wasomaji wa habari htafakari zaidi habari kuliko siku nyingine amabapo huzitrust habari zote kirahisi. na kama hilo ni kweli, inawezekana basi siku hii ndiyo siku pekee ya werevu na zilizobaki zote katika mwaka ndizo siku halisi za wajinga.
mfano habanri ya Tendwa kishukia CCJ/Mpendazoe, aikuwa na sifa yoyote ya kuitwa habari, na yoyote mwente tafakari hata ndogo tu angegundua ni a kutunga. sasa huoni kuwa imetoa changamoto kwa wale walioingia mkenge kuwa siku nyingine watafakari kila habari?
anagalia magazeti kaa ya udaku na hata baadhi ya magazeti yasiyo ya udaku. utagundua kuwa habari makini ni chache sana. sasa wale wanayoyaamin hayo magazeti huoni wanapaswa kuonywa watafakari kila habari?
ni maoni yangu ndugu