Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kujitoa kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), kwa vile imeona hakuna mantiki ya kuingia kwenye muungano mwingine wa nchi tano, kabla ya kutatua matatizo ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Taarifa hiyo ya serikali ambayo gazeti hili lina nakala yake imesema "kwa kuwa muungano wa EAC ni wa nchi tano, kuondoka kwa nchi moja hakutawazuia wale wengine wa nchi nne kuendelea na muungano huo".
Wachambuzi wa mambo wanasema kujitoa kwa Tanzania kumetokana na kuzinduka kwa Chama cha Mapinduzi, chama tawala tanzania, ambacho majuzi kilifanya mkutano mahususi kujadili hatima ya Jamhuri ya Tanzania kwenye muungano wa EAC, kwamba Tanzania ina rasilmali nyingi na haina haja ya kujiunga na EAC.
"Ushirikiano wa kikanda si lazima uwe EAC, sisi tuko SADC. Wenzetu wako IGAD. Zote hizo ni taasisi za ushirika wa kikanda, sehemu ya taarifa inasema.
SOURCE:
http://www.jamboleo.co.tz