Kuvuja kwa paper sio issue kwa mtazamo wangu. Hata tulipokuwa mashuleni paper zilikuwa zinavuja na wengine haziwafikii lakini bado wanafaulu, ni suala la kujiandaa na kujiamini tu.
Tatizo langu kwa nssf ni kuita watu interview kwa kuwatumia sms alhamisi tarehe 29/12/2011 na kutakiwa kufanya registration tarehe 30/12/2011. Sasa imagine mtu yuko mikoani huko kama Arusha, Mwanza, Mbeya na kwingineko, anawezaje kujiandaa kwa safari ndani ya kipindi kifupi kiasi hicho? hapa ni dalili za wazi kwamba kuna mchezo mchafu unachezwa, ili watu wengi wa mikoani wasifike, ili wenye ndugu na jamaa nssf wapate ajira kiulaini.
Na vile vile kuna tuhuma kwamba nssf inatoa ajira kwa kupendelea watu wenye imani fulani. Sasa hapo wasiwasi unazidi kuongezeka.