Aqua Power Tanzania Limited yafungua kesi ICSID ikidai Tanzania fidia ya bilioni 1.3 kisa kunyanyaswa na kunyimwa leseni miradi ya nishati

Sunday, October 11, 2015​


Mipango ya Jakaya Kikwete watanzania wapate simenti kwa bei nafuu, akamilisha mipango na kiwanda cha Dangote chazinduliwa


View: https://m.youtube.com/watch?v=WHjgF96lNXo

Sunday, October 11, 2015​

RAIS KIKWETE AZINDUA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE MTWARA​



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Halima Denengo na mmiliki wa kiwanda kipya cha Saruji cha Dangote Alhaj Aliko Dangote (nyuma yao) wakati wa sherehe za kuzindua kiwanda hicho kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara.


HISTORIA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KUVUTA UWEKEZAJI MKUBWA


Mjini Lagos nchini Nigeria alipotembela May 9, 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa baada ya kutembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014.



LAGOS, Nigeria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametumia siku nzima Ijumaa, Mei 9, 2014, kutembelea kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote duniani cha Dangote Cement Obajana Plant na kinachomilikiwa na tajiri mkubwa zaidi wa Afrika, Bwana Aliko Dangote, ambaye pia anajenga kiwanda kikubwa cha saruji mjini Mtwara.

Picha : Tajiri Dangote akimuonesha rais Jakaya Kikwete kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichoko katika eneo la Obajana, Jimbo la Kogi nchini Nigeria.


Akiandamana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Abdallah Kigoda, kwa siku nzima, Rais Kikwete ametembelea kiwanda hicho cha Saruji cha Dangote kilichoko katika eneo la Obajana, Jimbo la Kogi, kilomita 400 kaskazini mashariki mwa mji maarufu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos.


Rais Kikwete ambaye alikuwa nchini Nigeria kuhudhuria Kongamano ya Uchumi Duniani-Afrika (WEFA) mwaka huu aliamua kutumia siku yake ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini humo, kwa kutembelea uwekezaji mkubwa wa mwekezaji ambaye ameanza ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Mtwara ambacho kitakuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote katika Tanzania, kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani za kimetriki milioni tatu kwa mwaka.


Rais Kikwete ambaye amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kiwanda hicho na Bwana Dangote mwenyewe, ameanza ziara yake kwa kutembelea machimbo ya kiwanda hicho ambayo yako kilomita tisa kutoka kiwandani ambako malighafi ya kiwanda hicho husafirishwa kwa madaraja na mikada maalum hadi kiwandani.


Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kwa sasa Kiwanda cha Obajana kinazalisha tani za kimetriki milioni 10.25 kwa sasa kwa mwaka na hivyo kukifanya kiwanda hicho kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani kilichoko katika eneo moja na kuwa baada ya upanuzi unaoendelea kufanywa kwenye kiwanda hicho, uwezo wake wa uzalishaji utaongezeka na kufikia tani za kimetriki 13.0 kwa mwaka ifikapo mwakani 2015.


Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilicho kwenye eneo la kilomita za mraba saba kitakuwa kimegharimu kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.5 wakati upanuzi wake utakapokamilika. Kwa sasa kiwanda hicho kina biashara ya dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka.


Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilichoanza kujengwa mwaka 2003 na kukamilishwa mwaka 2006 na hatimaye kuzinduliwa na Rais Olusegun Obasanjo Mei 12, mwaka 2007, wiki mbili kabla ya kustaafu Urais wa Nigeria, kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja na hivyo kuwa miongoni mwa waajiri wakubwa zaidi katika Nigeria.

“Mheshimiwa Rais, ili kuelewa vizuri mchango wa kiuchumi na kijamii za kiwanda hiki na viwanda vyetu vingine katika maeneo mengine ya Nigeria, unahitaji kukumbuka kuwa kabla ya kuanza kujenga kiwanda hiki, Nigeria nzima ilikuwa na uwezo za kuwazalisha tani za kimetriki za saruji milioni1.5 tu, wakati huo chini ya miaka 10 iliyopita.

Tunataka kufikia hatua ya kuhakikisha kuwa eneo la Afrika Magharibi na hata Bara letu la Afrika linaacha kabisa kuagiza saruji nje ya Bara letu. Na tutafikia huko.”


Mbali na Kiwanda cha Obajana, Kampuni ya Saruji ya Dangote inazalisha saruji katika maeneo mengine mawili ya Nigeria ambalo uzalishaji wa jumla wa maeneo hayo matatu ni tani za metriki 20.25 kwa mwaka.


Amesema Bwana Dangote kuwa ili kuweza kuwa na uhakika wa umeme, uongozi wa kiwanda hicho uliamua kuzalisha umeme wake kwa ajili ya kiwanda hicho kwa kujenga, miongoni mwa hatua nyingine, bomba ya kilomita 92 la kusafirisha gesi kutoka Ajaokuta hadi kwenye kiwanda hicho.

Alipoulizwa na Rais Kikwete kama wanategemea kwa namna yoyote umeme wa taifa, Bwana Dangote alijibu kwa furaha, “hatujaunganishwa kwenye gridi ya taifa na tunadhani hili ni jambo zuri kwa sababu hatua tulizochukua zinatuhakikishia umeme wakati wote na kwa kiwango ambacho tunakihitaji.

Tunatumia gesi ama diseli yetu wenyewe. Na wala siyo umeme tu, hata miundombinu ya eneo hilo kiliwemo daraja hili kubwa linalonganisha eneo la machimbi na kiwanda, tumejenga sisi Mheshimiwa Rais.”


Bwana Dangote amesema kuwa mbali na kujenga miundombinu ya umeme wake, kiwanda hicho pia kimejenga bwawa lake lenyewe kwa ajili ya huduma ya maji kusaidia uzalishaji wa saruji bila kutegemea huduma ya maji ya Serikali. Aidha, bwawa hilo linatoa huduma ya maji kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho.

Mbali na shughuli za kiwanda, Kampuni ya Bwana Dangote inashiriki kwa karibu sana shughuli za jamii inayozunguka kiwanda ambacho kwa sasa imeanzishwa miji midogo saba katika eneo lililokuwa pori lenye nyumba 50 za wenyeji tu kabla ya shughuli za kiwanda hicho kuanzishwa.

Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inatoa shughuli za elimu, maji na umeme kwa wananchi ambao wanazunguka kiwanda ambacho tokea kuanzishwa kwake limevutia mabenki 13 ambayo yameanzishwa matawi yake katika eneo la kiwanda.

“Mheshimiwa Rais, mbali na nyumba za wafanyakazi, tunawajengea hata nyumba za kuishi wananchi wanaozunguka eneo hili ambao wanatuunga mkono sana.”


Mbali na kutoa huduma nyingine za kijamii, Kampuni ya Saruji ya Dangote inajenga taasisi kubwa ya elimu ya Dangote Academy ambayo itatoa elimu na mafunzo ya kiufundi kwa ajili ya kuandaa wafanyakazi wa kiwanda hicho na watoto wa jamii inayozunguka kiwanda hicho.

Ili kuhakikisha kuwa upanuzi wa kiwanda hicho unakwenda kwa kasi kubwa zaidi, Bwana Dangote ameagiza kiasi cha malori 6,000 kutoka China kusaidia ujenzi na pia amechukua uamuzi usiokuwa wa kawaida wa kuagiza maelfu ya vibarua kutoka nchi hiyo hiyo ya China kushiriki katika ujenzi huo na kuumaliza kwa haraka.


Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inafanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa Rais Kikwete anakifungua kiwanda cha saruji cha Mtwara kabla ya kustaafu mwishoni mwa mwaka ujao.


Mbali na Nigeria na Tanzania, Bwana Dangote ana viwanda ama anajenga viwanda vya saruji ama na shughuli za saruji katika nchi 14 za Afrika ikiwamo Ethiopia, Zambia, Mozambique, Kenya, Senegal na Sierra Leone, Afrika Kusini, Congo (Brazzaville), Cameroun, Ghana, Liberia na Ivory Coast.

Mbali na shughuli za uzalishaji wa saruji, Bwana Dangote ambaye anakubaliwa kuwa tajiri mkubwa zaidi katika Afrika kwa thamani ya dola za Marekani bilioni 25 yeye na kampuni yake ya Dangote Group pia ina shughuli za uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa chumvi, utengenezaji wa magunia, uzalishaji maji, uzalishaji wa vyakula vya aina mbali mbali, uzalishaji wa mafuta ya kupikia, utengenezaji wa nyanya. Kwa sasa anaendelea na ujenzi wa kiwanda cha mbolea na kile cha kuzalisha bidhaa za petrol na kemikali.


Kampuni ya Saruji ya Dangote – Dangote Cement- ndiyo kampuni kubwa kuliko zote katika Afrika Magharibi kwa sasa ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 22.7 kwa tathmini ya mwaka huu baada ya kuongeza thamani yake kutoka dola za Matrekani
bilioni14.5 za mwaka jana.


Mwishoni mwa ziara hiyo yenye mafanikio makubwa, Rais Kikwete ameondoka Obajana kurejea nyumbani kupitia Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Luanda, Angola ambako kesho (jumamosi) anatarajia kukutana na marais wa nchi hiyo kabla ya kurejea nyumbani.
 
Rais John Magufuli kaingia na mipango yake, TPDC mwaka 2018 tarehe 20 Agosti


View: https://m.youtube.com/watch?v=ziJbTgFmbFkKiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara kimeingia mkataba na Shirika la Maendeleo Nchini (TPDC) ya kuanza kutumia gesi inayozalishwa na shirika hilo ikiwa ni hatua ya utekelezaji mkakati wa kuviwezesha viwanda nchini kutumia nishati ya gesi katika uzalishaji ...
 
2017 14 March

AGIZO LA RAIS MAGUFULI

Agizo la Rais Dk. John Magufuli la kutaka Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania 'TPDC' kukamilisha makubaliano na kampuni ya Dangote Group of Industries juu ya bei ya mauziano ya gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya kiwanda hicho cha kutengeneza saruji kilichopo Mtwara limetekelezwa.


View: https://m.youtube.com/watch?v=L4bFUDvkvFo
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa TPDC, Bw. Kapuulya Musomba amesema wamekubaliana juu ya kuunganishwa miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa la gesi kwenda kwenye kiwanda cha Dangote pamoja na kukamilisha mkataba wa awali kwa ajili ya mauziano ya gesi kwa matumizi ya kiwanda hicho.
 
Wameshajua panapovuja wapi..
Pia mikataba walisaini gizani na viongozi wetu walitudanganya kuwa ni siri ila sasa madeni sio siri yapo hadharani.
Tuna ujinga mwingi sana.
 
kikomunisti, ndio maana unaona hata raia matajiri wengi Sana kutoka nchi Kama Urusi au China wanazikimbia nchi zao na kwenda kuwekeza kwenye nchi zingine zisizokuwa na itikadi za ukomunisti. Wanafikiri matajiri hao ni wajinga??

Hao matajiri wa Kichina na Kirusi wanaokimbia nchi zao za Kikomonisti walipatia wapi huo utajiri, kwa mabepari ???
 
Rais Magufuli Aingilia kati kukata, alichoita mizizi ya wapiga dili
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote
Dar es Salaam.
10 Desemba, 2016.



View: https://m.youtube.com/watch?v=Jxa2FZUA-Tg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.


Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.

Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.

''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili '' amesema Rais Magufuli.

Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43 kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.

Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.

Katika kuthibitisha hilo, tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.

Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania na kamwe hana nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.



Source :
Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.
10 Desemba, 2016.
 
Hao matajiri wa Kichina na Kirusi wanaokimbia nchi zao za Kikomonisti walipatia wapi huo utajiri, kwa mabepari ???
Ni ukweli. Mie na rafiki zangu huwa wananiambia kuwa wanapigiwa simu na maofisa hata mawakili wa Tanzania kuwauliza kama wanaidai serikali ya Tanzania watawasaidia kupata pesa. Hapo huwa sielewi kwa vipi wanapata huo mwanya wa kuiba na sheria tunazo.

Ni system zima iliyojipanga - Laywer - Judge(hakimu) inawezekana hata prosecutors. Uozo kabisa.
 
Hao wapiga deal ni akina nani?
 
Maamuzi ya mtu mmoja kwa kutoa tamko ni hatari sana kwa uchumi wa nchi.

Nchi inahitaji kuaminika, siyo mtu mmoja Ikulu ndiye awe ameandaa mambo ya nchi kwa mtizamo wake bila ushirikishwajwi umma kupitia visheni ya kiuchumi ya muda mrefu.

Pia taratibu ziwe wazi kuwekwa katika media wananchi wafahamu kwa kina nini kinaendelea. Miradi mikubwa siyo mali ya mtu binafsi, hivyo viongozi wawe makini kushirikisha umma.
 
1. Uwazi na Demokrasia siyo Sera Wala siyo utamaduni wa Watawala wenye itikadi ya Ukomunisti/Ujamaa.

Wakomunisti sera na tamaduni zao ni Usiri uliopitiliza ambao hauna UMUHIMU na Wala hauna maana. Mambo ambayo yanatakiwa kubaki kuwa Siri wao huwa wanayaweka hadharani Kama matangazo, na yale mambo ambayo yanatakiwa yawe wazi kwa umma wao huwa wanayaficha na kuwa Siri.

2. Sera na Itikadi za Ukomunisti/ujamaa zinaamini kwamba Mwenyekiti ndiye mtu pekee kabisa katika nchi ambaye ana akili kubwa zaidi na mwenye maono na akili nzuri zaidi kuliko mtu mwingine yoyote yule. Hivyo, fikra zake zinapaswa kudumishwa na kuenziwa kutoka kizazi kimoja hadi lingine.
3. Aidha, Sera na Itikadi za Ukomunisti/ujamaa zinaamini kwamba Watu/Aananvhi wote waliopo kwenye ni wanachukuliwa Kama Mateka tu Mwenyekiti.
 

Tatizo siyo maamuzi ya mtu mmoja, rushwa, CCM, Chadema wala nini….tatizo ni WB na hiyo ICSD.
Matt Kennard ana kitabu kabisa kuhusu hii mambo, kinaitwa “How Corporations Overthrew Democracy.” Pia aliandika makala the guardian, naweka link hapo chini. Ukipenda zaid, msikilizi ana video nyingi tu YouTube kuhusu huu ujambazi na topics nyingine..

 
Tundu Lisu vs Tigo Hororo millcom 😂😂
Yaani ukipigwa risasi Tanzania is an investment dispute. Ukinyimwa kuwekeza Tanzania is an investment dispute. Hata ukinyimwa unyumba Tanzania is an investment dispute. Wote mnaweza kuishitaki Tanzania huko International Court for Settlement of Investment Disputes, Washington na mkashinda kesi kirahisi na mkaruhusiwa kukamata ndege za ATCL mkizikuta popote duniani.
 
My Take: Hizi kampuni za Matapeli zipigwe marufuku na Wale Wanaoshirikiana Wasakwe Popote Nchini Ili Wafurushwe hata kama Ni Watanzania.

Huu umegeuka ni upuuzi na dili za Vibaraka wa Mabeberu 👇👇
Mkuu ukichunguza walifikaje hadi kuingia mikataba utakuta ni hawahawa wenye dhamna ya kuongoza nchi (ccm) ndio wanawaleta na kulea huu upuuzi!
 
Mkuu ukichunguza walifikaje hadi kuingia mikataba utakuta ni hawahawa wenye dhamna ya kuongoza nchi (ccm) ndio wanawaleta na kulea huu upuuzi!

Kila rais anayeingia ikulu anajimwambafai kwa kuvuruga miradi iliyoanzishwa ktk awamu iliyopita kiasi hakuna miradi ikawa endelevu kuenea nchi nzima.

Dangote alitaka kuanzisha viwanda vingine Tanzania ikiwemo kiwanda cha mbolea lakini amesita kutokana na kuona marais wa Tanzania wakikanyagana kuua mazingira rafiki yaliyowekwa na mtangulizi wake Ikulu matokeo miradi zaidi haianzishwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…