Archbishop Janan Luwuum and President Idd Amin Dada

Wema gani?mayala mbona kama hujielewi,kwani sheria alitunga nan namahakama zenu na kanuni sibungelenu laccm?walishawambia kwann hamtaki kumpeleleza kwanza ndipo mkamate MTU,muwatese wenyewe ,tena urudi useme unawaonea huruma!!!!hapa ndipo tunapishana sana.... Hivi viini macho kwasasa havina nafasi.tatizo mtengeneze wenyewe harafu mtuzunguke huruma.
 
Kuna ushahidi usio na shaka kuwa Iddi Amin aliagiza huyo mtu auawe au ni western media pamoja na wasiompenda Amin kumchafulia jina tu kwa sababu alizingua maslahi yao?
 
Hiyo barua ya Maaskofu imeanza kuniaminisha kuwa huenda chuki ya Nyerere kwa Amin pamoja na mambo mengine ilikuwa na component za Kidini pia.

Kwenye hiyo barua maaskofu wanamlaumu Amin kuwa serikali yake inapendelea "Waislamu"

Tukirudi kwenye Pattern za utawala wa Nyerere, tunagundua kuwa Nyerere mkatoliki miaka nyuma kabla ya vita vya Kagera anaamua kuliunga mkono jimbo la Wakiristo wakatoliki wenzie wa Biafra lijitenge kutoka nchi ya Nigeria kwa madai kuwa Serikali ya Nigeria ambayo wakati huo ilikuwa ikiongozwa na waislamu wengi kuwanyanyasa!

Lakini kabla hatujakaa sawa kuna movement inayoongozwa na kanisa Katoliki huko Uganda kumfanya Nyerere "Mtakatifu" na Museveni anapigia chapuo atangazwe mtakatifu!

Ukiacha Geopolitics Nyerere alikuwa too loyal kwa kanisa lake Katoliki na alilifanyia kazi nzuri sana Tanganyika na Tanzania kwa mbinu na usiri wa hali ya juu bila kuacha traces za kubackfire!
 
Idd Amin pia alikuwa loyal kwa dini yake. Kabla ya Amin kuingia madarakani Uislam ulikuwa 5% ya population. Utawala wa Amin karibu Magenerali wote wa jeshi walikuwa watu wa dini na kabila lake.

Ninakumbuka usemi wake mmoja alisema Mwarabu akikupa msaada ni kama sadaka lakini Mzungu akikupa msaada atataka kitu kwako na unaweza kulipa mara mbili. Hapa ni wakati ameanza kuwategemea Waarabu kwa misaada.

Baada ya jaribio la kumpindua mwaka 1972 kushindwa , Amini aliwaua wanajeshi wa Kabila la Obote kama kuku.

Kumsafisha Amini na kasha’s ya mateso na mauwaji ni ngumu sana mkuu ila ana mazuri yake ingawa mabaya yalikuwa mabaya mno kizazi cha kufunika kabisa mazuri yake.
 

Sasa kama askari wanashiriki kutaka kupindua serikali adhabu yao nini?

Uhaini salama yake mfanikiwe kushika dola, mkishindwa risasi ni halali yenu!

ulichosema kuhusu Amin kupenda dini yake ndo exactly nilichokuwa nakizungumza mimi, kuwa huenda Mkatoliki Nyerere hakupendezwa kabisa na Islamization of Uganda!

Uganda siku zote imekuwa nchi ya Kikabila, Obote alipendelea kabila lake, na leo Museveni the same
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…