Ardhi si mali ya Muungano-Zanzibar hairuhusu Watanganyika kumiliki ardhi visiwani

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Ardhi si mali ya Muungano:

"Mwanasheria anena na JAMHURI"

"Sheria ya Ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992 hairuhusu mtu asiye Mzanzibari (wakiwamo Watanganyika) kumiliki ardhi Zanzibar."

Wazanzibari wanajidanganya kama wanakimbia kununua ardhi katika maeneo mbalimbali ya Tanganyika , kwani watapoteza fedha zao bure.

¡°Bila hata kubadili sheria ya sasa, kitakachobadilika katika sheria za ardhi Na. 4 na Na. 5 za mwaka 1999 ni jina kutoka Tanzania kwenda Tanganyika.

Sheria iko wazi, kuwa mtu ambaye si Mtanganyika ataruhusiwa kupewa ardhi ya Tanganyika iwapo tu anafanya kazi ya uwekezaji.

¡°Inatamka wazi kuwa ardhi ya Tanganyika si kwa ajili ya watu kuja kujenga makazi, bali uwekezaji. Hivyo kama kuna Mzanzibari anayejidanganya kuwa akinunua ardhi Tanganyika atajenga na kuishi hapa kama si mwekezaji anapoteza kuda na fedha zake.

Ardhi hiyo itachukuliwa na Rais wa Tanganyika bila kulipwa fidia. Wazanzibari wameyataka haya, lazima tuelezane ukweli mgumu,¡±

¡°Umiliki wa ardhi, haki za wenyeji na mipaka ya matumizi ya ardhi kwa wageni utawekwa wazi."

Na sasa wageni ni pamoja na Wazanzibari. Nasema Tanganyika wana haki ya kutunga sheria yao na wana haki ya kuweka mipaka kwa walio wageni.

¡°Wageni hawatapewa haki ya kumiliki ardhi ila watakuwa na haki ya kutumia ardhi. Zanzibar kilichowapa access (umiliki) wa ardhi ya Tanganyika awali ni kwa sababu sisi Tanzania Bara imo ndani ya Muungano. Itabidi Wazanzibari wajue kuwa nao ni wageni wakija Tanganyika."

¡°Tuliwatahadhalisha na tunaendelea kuwatahadharisha kuwa hata ukinunua ardhi Katiba ya Tanzania Bara (Tanganyika) itakuwa na haki ya kufuta umiliki wa ardhi."

"Mzanzibari atatumia ardhi kama mwekezaji ila si makazi, au kilimo cha kujikimu."

¡°Ni kama ambavyo Wakenya wanakuja wananunua ardhi na nyumba kumbe wanapoteza fedha zao, hata wakikimbilia kununua wanapoteza hela zao bure,¡±

Sheria ya Ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992 hairuhusu mtu asiye Mzanzibari (wakiwamo Watanganyika) kumiliki ardhi Zanzibar.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, alipoulizwa na JAMHURI juu ya mshikemshike wa ardhi na kuhamishwa kwa makao makuu ya Serikali ya Tanzania kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, alisema kwa ufupi, ¡°Mawazo haya yalikuwapo na yalizungumzwa, ila tusubiri wananchi ndiyo waamue.¡±

Tafsiri rahisi juu ya mabadiliko haya ina maana Wazanzibari waliojenga Tanganyika wanaokadiriwa kufikia 600,000 wanaweza kulazimika kurejea Zanzibar kwanza na kurudi Tanganyika baada ya kuomba, ama kibali cha ukaazi, au uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kukubaliwa kupewa ardhi baada ya kutimiza masharti.

Moja ya masharti ya uwekezaji watakayopaswa kuyatimiza kupitia TIC ni kwamba lazima mwekezaji kama anataka kwenda kuwekeza Tanganyika awe na mtaji usiopungua dola 100,000 sawa na Sh milioni 160 za Tanzania ndipo apewe vibali vya kuishi. Wazanzibari wanaweza kutakiwa kutekeleza sharti hilo la kisheria.

JAMHURI
 
Ali Hassan Mwinyi
Samia Suluhu Hassan Mwinyi.
A coincidence?
Kuna jambo tofauti na ardhi unataka kulizungumzia kwani? Hakuna aliyekataa mtoto wala mimba, DNA ya nini sasa?

Jamaa wajinga sana, tupige chini muungano waone kama watatosha kwenye visiwa vyao, jwa ule wastani wao wa 1 kwa 9, wataishi kama wako K/koo
 
Siyo ardhi tu hata mgawanyo wa madaraka ni tofauti sana wazanzibar wanafanya lolote bara lakini mtu wa bara ukienda znz unawekewa mipaka
 
Huu Muungano wadanganyika tumekubali kupoteza vingi kwa ajili yake mpaka inaduwaza.. why???
 
Ardhi si mali ya Muungano:

"Mwanasheria anena na JAMHURI"

"Sheria ya Ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992 hairuhusu mtu asiye Mzanzibari (wakiwamo Watanganyika) kumiliki ardhi Zanzibar."

Wazanzibari wanajidanganya kama wanakimbia kununua ardhi katika maeneo mbalimbali ya Tanganyika , kwani watapoteza fedha zao bure.

¡°Bila hata kubadili sheria ya sasa, kitakachobadilika katika sheria za ardhi Na. 4 na Na. 5 za mwaka 1999 ni jina kutoka Tanzania kwenda Tanganyika.

Sheria iko wazi, kuwa mtu ambaye si Mtanganyika ataruhusiwa kupewa ardhi ya Tanganyika iwapo tu anafanya kazi ya uwekezaji.

¡°Inatamka wazi kuwa ardhi ya Tanganyika si kwa ajili ya watu kuja kujenga makazi, bali uwekezaji. Hivyo kama kuna Mzanzibari anayejidanganya kuwa akinunua ardhi Tanganyika atajenga na kuishi hapa kama si mwekezaji anapoteza kuda na fedha zake.

Ardhi hiyo itachukuliwa na Rais wa Tanganyika bila kulipwa fidia. Wazanzibari wameyataka haya, lazima tuelezane ukweli mgumu,¡±

¡°Umiliki wa ardhi, haki za wenyeji na mipaka ya matumizi ya ardhi kwa wageni utawekwa wazi."

Na sasa wageni ni pamoja na Wazanzibari. Nasema Tanganyika wana haki ya kutunga sheria yao na wana haki ya kuweka mipaka kwa walio wageni.

¡°Wageni hawatapewa haki ya kumiliki ardhi ila watakuwa na haki ya kutumia ardhi. Zanzibar kilichowapa access (umiliki) wa ardhi ya Tanganyika awali ni kwa sababu sisi Tanzania Bara imo ndani ya Muungano. Itabidi Wazanzibari wajue kuwa nao ni wageni wakija Tanganyika."

¡°Tuliwatahadhalisha na tunaendelea kuwatahadharisha kuwa hata ukinunua ardhi Katiba ya Tanzania Bara (Tanganyika) itakuwa na haki ya kufuta umiliki wa ardhi."

"Mzanzibari atatumia ardhi kama mwekezaji ila si makazi, au kilimo cha kujikimu."

¡°Ni kama ambavyo Wakenya wanakuja wananunua ardhi na nyumba kumbe wanapoteza fedha zao, hata wakikimbilia kununua wanapoteza hela zao bure,¡±

Sheria ya Ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992 hairuhusu mtu asiye Mzanzibari (wakiwamo Watanganyika) kumiliki ardhi Zanzibar.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, alipoulizwa na JAMHURI juu ya mshikemshike wa ardhi na kuhamishwa kwa makao makuu ya Serikali ya Tanzania kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, alisema kwa ufupi, ¡°Mawazo haya yalikuwapo na yalizungumzwa, ila tusubiri wananchi ndiyo waamue.¡±

Tafsiri rahisi juu ya mabadiliko haya ina maana Wazanzibari waliojenga Tanganyika wanaokadiriwa kufikia 600,000 wanaweza kulazimika kurejea Zanzibar kwanza na kurudi Tanganyika baada ya kuomba, ama kibali cha ukaazi, au uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kukubaliwa kupewa ardhi baada ya kutimiza masharti.

Moja ya masharti ya uwekezaji watakayopaswa kuyatimiza kupitia TIC ni kwamba lazima mwekezaji kama anataka kwenda kuwekeza Tanganyika awe na mtaji usiopungua dola 100,000 sawa na Sh milioni 160 za Tanzania ndipo apewe vibali vya kuishi. Wazanzibari wanaweza kutakiwa kutekeleza sharti hilo la kisheria.

JAMHURI
Hiyo ndiyo sheria aidha Katiba au Sheria za Ardhi Na.4 na Na.5 zisemavyo! Lakini uhalisia UKOJE? Hilo ndilo muhimu, haya mengine ni blaah blaah tu!
 
Back
Top Bottom