Ardhi Special thread

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
6,585
Reaction score
10,363
Habari wana JF

Karibuni kwenye Ardhi special thread huku tutapeana taarifa mbali mbali kuhusiana na Umiliki wa viwanja na Mashamba

Pia tutapeana njia mbali mbali za kufanikisha maswala ya umiliki wa viwanja Mijini na vijijini

Tutapeana mbinu mbali mbali za kuepuka kutapeliwa

Upande wa hati miliki tutapeana elimu za namna ya kupata Hati miliki

Utofauti wa kati ya hati miliki ya wizara, hati miliki ya kimila na hati miliki ya serikali ya mtaa

Karibuni tuchangie mada , Kama kuna mtu ana swali analohitaji ufafanuzi wake aulize hapa naimani atapata majibu yake

Asanteni
 
Nipo Live kuwasoma wajuvi 😚
 
Ardhi kubwa nchi hii haina hati, nina kiwanja Dodoma, toka 2018 nafuatilia hati, control number tu ni shida. Na kujenga lazima upewe kibali, kibali lazima uwe na hati. Kero ni nyingi sana kwenye kupata hati miliki
 
Ardhi kubwa nchi hii haina hati,Nina kiwanja dodoma,toka 2018 nafuatilia hati,control number tu ni shida.Na kujenga lazima upewe kibali,kibali lazima uwe na hati.kero ni nyingi sn kwenye kupata hati miliki
Mbona naona siku hizi swala la kupata Hati miliki limekua rahisi Especially sehemu za miji mikubwa

Mfano hapa dar es salaam makampuni mengi ya real estate yanawasaidia clients wao katika kufuatilia Hati
Me nafkiri Hati miliki ukifuatilia mwenyewe bila ya kuwa na mtu wako wizarani kidogo itakua mtiani
 
Ardhi kubwa nchi hii haina hati,Nina kiwanja dodoma,toka 2018 nafuatilia hati,control number tu ni shida.Na kujenga lazima upewe kibali,kibali lazima uwe na hati.kero ni nyingi sn kwenye kupata hati miliki
Mimi pia nipo Dodoma, ila Hati nimeipata ndani ya mwezi mmoja tu tokea nianze kuifuatilia' control number nilipewa siku hio hio, kibali sio lazima uwe na hati' kibali ukiwa tu na invoice unapewa ndani ya 1 week!!
 
Nashindwa kuelewa jamaa atakua amekwama wapi
Hati siku hizi sio issue kabisa
 
Tuko pamoja kwenye hili
 
Wakuu naona njia rahisi ya kubadili jina kwenye hati,nimenunua kiwanja huu mwaka wa pili........kimepimwa,ikiwezekana na makisio ya gharama zote
Watakuja wenye ujuzi wakupe muongozo
 
Ardhi kubwa nchi hii haina hati,Nina kiwanja dodoma,toka 2018 nafuatilia hati,control number tu ni shida.Na kujenga lazima upewe kibali,kibali lazima uwe na hati.kero ni nyingi sn kwenye kupata hati miliki
hili la kujenga kuwa lazima uwe na hati si kweli, vibali vinatolewa kwa maeneo yaliyopimwa pia kwa yasiyopimwa, kwa eneo lililopimwa na hati haijatoka utapewa kibali kupitia offer ya eneo husika na kwa yasiyopimwa kibali kinatolewa kupitia mkataba wa mauziano ulioidhinishwa na serikali ya mtaa/kijiji husika.
 
Lakini kwa dunia ya sasa ni vizur zaid kuwa na Hati miliki ili kuepusha migogoro ya Ardhi
 
viwanja vilivyopimwa huwa na bei kubwa hivyo wengi wetu hushindwa kumudu gharama zake. ila unaweza nunua eneo hata lisilopimwa baada ya kujua matumizi ya eneo husika na kufanya upimaji baadaye.
Uko sahihu ila ni muhimu kununua kutoka kwa makampuni ya real estate kuliko kununua kwa mtu binafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…