Ardhi tunayo, tumekosa siasa safi na watu kupiga hatua

Ardhi tunayo, tumekosa siasa safi na watu kupiga hatua

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
441
Reaction score
1,065
Iliwahi kutajwa kuwa ili tuendelee tunahitaji ardhi, siasa safi na watu. Ardhi ipo hadi yakumwaga, siasa ipo hadi vyuo vikuu isipokuwa imekosa maji na sabuni ili ioshwe iwe safi na hii ni kwasababu nchi haina "watu" wenye uwezo wa kuiosha na kuondoa madoa sugu yaliyoachwa na yanayoendelea kuwekwa na wakoloni

Nchi imekosa watu wanaofikiria nchi, watu wanaotamani kuendeleza nchi,watu wanaotamani kukumbukwa,watu wenye damu ya uzalendo na haina watu wanaotamani kuwa watu kweli.

Mtu ni yule anayejithamini, anayejiamini, anayejitegemea, anayependa vyake, anayefikiri na kuamini fikra zake, anayejikubali na kuamini anaweza, anathamini utu wa mwingine, anayefurahia furaha na amani ya mwingine

Wakoloni waliondoa utu wa mwafrika na hivyo waliondoa karibu sifa zote za mtu kuwa mtu.

Waliopigania uhuru walitaka turudi kuwa watu lakini tuliowapa madaraka wamekataa tusiwe watu.

Hawataki tufanye vitu vyetu wenyewe, tukifanya hawaviamini. Hawataki tufikiri wenyewe, fikra zetu wanaziita uharifu na upinzani. Hawataki tuwe watu, hawataki tuendeleze nchi kwasababu nchi inahitaji watu ili iendelee.

Tutakuwaje watu endapo bado walioondoa utu wetu bado tunawaruhusu watengeneze mitaala yetu ya elimu,watunge sera zetu na kuendesha siasa zetu? Hii maana yake ni kuwaruhusu kutengeneza watu wanaowahitaji wao kwa manufaa yao sio wanaohitajika na nchi

Watu wanahitajika sana kuweza kutumia ardhi na siasa. Swali linabaki ni lini hao watu watapatikana?
 
Back
Top Bottom