Argentina yapitisha muswada wa kuhalalisha utoaji wa mimba

Argentina yapitisha muswada wa kuhalalisha utoaji wa mimba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Baraza la seneti la Argentina, limepitisha mswada wa sheria wa kihistoria unaohalalisha uavyaji mimba katika taifa ambalo Kanisa Katoliki limekuwa na ushawishi mkubwa kwa muda mrefu.

Argentina imekuwa miongoni mwa kundi dogo la nchi za Amerika Kusini kuchukua hatua hiyo.

Muswada huo ulipendekezwa na Rais Alberto Fernandez na ulipitishwa katika mabaraza ya chini Desemba 11, licha ya upinzani mkali kutoka katika Kanisa Katoliki na makanisa ya Kievanjelisti.

Serikali ya Argentina inasema kati ya visa 370,000 na 520,000 vya uavyaji mimba kinyume na sheria hurekodiwa nchini humo kila mwaka, katika taifa hilo lenye watu milioni 44.

Miaka miwili iliyopita, muswada kama huo ulipitishwa katika mabunge ya chini, lakini ukaangushwa baadaye katika baraza la seneti.

Muswada huo unawaruhusu wanawake kuavya mimba, hadi muda usiopita wiki 14 tangu kupata ujauzito.
 
Kuna nchi unaweza kudhania hawaishi watu walioumbwa na Mungu, yaani wanafanya maisha kwa mazoea tu kana kwamba wangefanyiwa wao sijui wangekua wapi...! Ukute huyo rais ni ana kashfa ya kunyanyasa kingono ladies na ameshatia mimba kadhaa na wamemtishia kumshtaki hivyo kaona awahi kulegeza nati juu kwa juu kuepuka fedhea... (Nimewaza hivyo tu lakini) 😎
 
Back
Top Bottom