Kilimo kwanza!!!!!!! halafu what next ie ......pili
Anyway tanzania imekuwa ikiendeshwa na kilimo toka tumepata uhuru. Kilimo cha jembe la mkono ndicho kilichosomesha majority ya watanzania, mbolea hamna na kama ilikuwepo basi kidogo sana na wakati wote sikuwahi kusikia kuwa kuna njaa tanzania na au tunaagiza chakula toka nje.
Tulisoma kuwa uchumi wa tanzania unatokana na chai, pamba, kahawa tumbaku ambayo in reality haikulimwa na settlers zao pekee lililolimwa na settlers ni mkonge na tumbaku kidigo sana, zao la mkonge na settlers wa tumbaku waliondoka baada ya azimio la Arusha na kufanya mazao hayo yaendeshwe na wananchi walalahoi na bado kilimo kiliendelea kuendesha nchi kwa biashara na chakula.
Tunaposema leo kilimo kwanza naona kizunguzungu, labda ndio maana mwanakijiji na jembe lake amedisappear, look at theso called big four regions kilimo chao bado ni kilekile cha kizamani yule tajiri ni mwenye kambaku ( ng'ombe dume) na plau ya kizamani kwani ufi na zzk sasa hivi kwisha kazi.
inakuja idea ya power tillers eti ndo solution na au kichocheo cha kilimo kwanza, mafundi tunao, mafuta tunayo vijijini do they need such advanced things bila hata kuwatayarisha. Ardhi wanayo jee serikali inaithamini ardhi wanaweza kuitumia kama collateral, kwa mfano serikali ilileta kitu kinaitwa lleseni za makazi ambayo walisema itakuwa kama title nyingine mpakaleo benki zinakataa leseni za makazi kama collateral.
Lets go back to the drawing board and see how we can improve the lives of our poor, forgotten and neglected farmers we should ask them what they need to emancipate themselves na sio sisi kuwapa terminologies tamu ambazo kwao ni kizunguzungu.