Armed robbers raid Mwadui diamond

sijui hii ya tansort iliishia wapi. tansort inamilikiwa 100% na serikali lakini watu wachache sana (ni akina nani?) wana access na vitabu vyao vya mahesabu masikini tanzania yangu


source the eastafrican january 23, 2006 http://www.nationmedia.com/eastafrican/23012006/News/news230120063.htm
 
oops, naona quote hapo juu itawasumbua watu kusoma. samahani kwa usumbufu.
 
..kitila,

..ideas zilizotolewa,hasa nawe,ni nzuri. tatizo lipo katika utekelezaji!

..kwa mfano,leo hii ukisema yule jamaa hafai kabisa mtaani ni jambazi tena linaua,hebu tulivizie tuliue[sorry for this!],watu watakuitikia na kutoa michango lumbesa!tatizo ni kuwa usiku saa mliyokubaliana unaweza jikuta uko peke yako!

..its frustrating all the time!

..at times dictatorships are good,for the good cause!i'm thinking of pakistani right now!,if only i can erase the recent happenings!
 
ni taarifa za kutisha ambazo nilikua nazo tokea asubuhi, lakini kwa sababu za kitaalamu nililazimika kuanzisha hii mada kiana.
 
..na hasa ukizifikiria kwa kina!

HAswaa Dar si Lamu.... maana hili li nchi... japo sikujua kwamba hata zile 25% zilikwisha kuuzwa kwa bei cheeeeeee
 

Mkuu Halisi hii ni habari nzito sana...

Asante sana kwa kuitoa maaana muda wote nilikuwa nasoma hii thread kusubiria hii breaking news.

Nashukuru kwa kazi nzuri mnayoifanya huko Tanzania.

Kwa kweli mungu awalinde na kuwatunza wenzetu mnaorisk kila kitu ili kutupatia hizi documents.
 
Admin,

Naomba hii thread ibadilishwe title kuwa hilo ambalo Halisi amelitumia sasa hivi kuwa ni breaking news ya wizi katika mgodi wa Mwadui
 
HAswaa Dar si Lamu.... maana hili li nchi... japo sikujua kwamba hata zile 25% zilikwisha kuuzwa kwa bei cheeeeeee

..kilevi chako[si lazima iwe pombe!ila be careful!] ni nini?...usitoe jibu,si lazima!

..basi kishikilie kikuliwaze!kwa kuwa hii inatia simanzi haswa!

..itakapofika siku[utaijua,utajulishwa au na kuwajibishwa!]zinduka kwa ulevi,reboot,halafu kata nyasi na magugu hali kadhalika kama huna akili nzuri!ukijasimama and look back,at least utakuwa happy,you did play your part!

..ipo siku.....hata wadai uhuru babu zetu walisema[japo wengine walikufa bila kuuona!]
 
Admin,

Naomba hii thread ibadilishwe title kuwa hilo ambalo Halisi amelitumia sasa hivi kuwa ni breaking news ya wizi katika mgodi wa Mwadui

..are we 100% sure this is breaking news!

..its not like i'm doubting halisi,but,utamu utapungua kama itakuwa na mapungufu ya kuiita breaking news!

..all in all,it's something big,if it's what it is!
 
Haya waheshimiwa, THISDAY lililopotea katika mtandao hiloo limeibuka tena na kwa hili sasa wametupa nguvu ya kusema kweli its Breaking News. Nadhani sasa polisi na uongozi wa mgodi wa Mwadui watatoa taarifa rasmi leo. Hebu tusubiri lakini wasije kwenda kuwapiga risasi wananchi wa maeneo ya Maganzo, Idukilo, Kishapu, Muhunze, Kolandoto na maeneo mengine jirani kwani hii inatisha shaka kama watu wa ndani ya mgodi hawahusiki maana kawaida watu wa maeneo jirani wizi wao mkubwa ni mchanga unaomwagwa maeneo jirani na uzio na huwa wanachota mchanga bila kuwa na uhakika kuna nini ndani. Hao wa jana wameingia na kuchukua almasi tena ndani. Nakumbuka niliwahi kuambiwa kwamba sorting kuna camera za usalama na watu wakiingia na kutoka wanapekuliwa kwa kiwango cha juu.

http://www.thisday.co.tz/News/3079.html


 
..nakuheshimia!

..sasa hapa biashara ya private security companies ndio itakuwa vizuri!

..halafu,ndio tuna aminishwa kuwa hawapati sana almasi au? kwa anayejua bei,hivi carat 1 ni bei gani?kwa soko la kimataifa?
 
Kuna mtu anasema kati ya USD 220 hadi 280 lakini na yeye ni kwa kutumia uzoefu katika biashara ya almasi, huko Shinyanga na Mwanza.. Kwa wanaoweza kupata katika masoko rasmi ya kimataifa watuwekee.
 
I wish walioiba wawe ni waTz waliochoka kuibiwa na hao makaburu. atleast wataenda kujiliwaza wao na familia zao za KITANZANIA.Kuna wakati ule mgodi wa buhemba kuliibiwa gold 90kgs, wezi walijulikana na hata polisi waliwajua lakini hadi leo hawajakamatwa. why. because watu wamechoka kunyanyaswa na wageni wanaofaidi raslimali zetu huku wao wanaishi maisha magumu. so its better waibiwe as long as watakaofaidi ni wanyonge na pesa zitabaki nchini. Thats what I think.
 

Wazo lako Judy, lina utata mkubwa maana hatupendi kutetea kuvunja sheria.. Lakini kuna maswali ya kujiuliza, Tanzania kwa miaka zaidi ya 40 hatujafaidi chochote katika mgodi wa Mwadui na sasa haya hospitali iliyokua ikihudumia watu sasa haipo, hata uwanja wa ndege uliokua ukitumika sasa haupo, lakini pia hata mapato hayajulikani na zaidi hao hao wageni ndio wananufaika na baadaye wanajiibia wenyewe kwa wenyewe na Watanzania wanaozunguka wanaambulia kuzamishwa kwenye madimbwi ya tope pale katika maeneo yanayozunguka mgodi huo... Hapo ndipo jibu la wacha waibe ama wasifanye dhambi hiyo linakua tata kidogo... Ndio maana hata hoja ya majambazi wauawawe na kuchomwa moto kuna hakuna jibu la moja kwa moja inabaki, "INATEGEMEA NA MAZINGIRA" na hapa pia "INATEGEMEA NA MAZINGIRA YA TUKIO" hebu tusubiri tusikie.
 
Kuna mtu anasema kati ya USD 220 hadi 280 lakini na yeye ni kwa kutumia uzoefu katika biashara ya almasi, huko Shinyanga na Mwanza.. Kwa wanaoweza kupata katika masoko rasmi ya kimataifa watuwekee.

..my calc. inaniambia 280*50 ni 14000!

..ina maana on a good day zinapatikana millioni kama 16 na upuuzi hivi?[1 usd = 1170 tshs]

..kama ni kweli basi haulipi huo mshimo!sasa,wanakaa kungojea nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…