Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Orobaini za ATCL zatimia kwa Waziri
Stella Nyemenohi
Daily News; Thursday,January 29, 2009 @21:15
Kamati ya wataalamu iliyopewa kazi ya kuchunguza chanzo cha matatizo ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), imewasilisha ripoti yake serikalini na kutoa mwanya kwa Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kutoa uamuzi kulingana na mapendekezo yaliyomo.
Ingawa haikufahamika mara moja mapendekezo yaliyomo katika ripoti hiyo iliyokabidhiwa jana Dar es Salaam, lakini Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa alisema serikali ilikuwa ikiisubiri kwa hamu ripoti hiyo kwa ajili ya kuyatumia yaliyomo kutolea uamuzi unaolenga kuboresha kampuni hiyo.
Tulisuburi kwa hamu. Baada ya upembuzi wa kina, kazi yetu ya kuboresha ATCL itakuwa rahisi, alisema Dk. Kawambwa na kusisitiza kuwa baada ya uchambuzi, watatafakari na kuchukua uamuzi uliopendekezwa ndani ya muda mfupi.
Chini ya uenyekiti wa Profesa Idrissa Mshoro, kamati hiyo ilikuwa ikichunguza kwa kina, kubaini kwa ufasaha matatizo yanayoikabili ATCL na kutoa mapendekezo ya kutatua matatizo hayo. Waziri alisema ana imani mapendekezo yaliyotolewa hayajafungwa na kitu chochote kwa kuwa kamati hiyo siyo ya kichama na wala kiserikali, bali ni ya wataalamu na iliyokuwa huru katika uchunguzi wake.
Alisema kamati hiyo ilipewa muda mfupi wa siku 21 kufanya kazi hiyo kutokana na dharura ya suala lenyewe la kutaka mapendekezo ya kitaalamu ili kuboresha huduma za kampuni hiyo. Timu ilitumia siku 28 badala ya ilizopewa kutokana na kile alichosema Waziri kwamba ni ugumu wa kazi yenyewe.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Mshoro alisema watu 56 kutoka maeneo tofauti walihojiwa. Vile vile wamepitia nyaraka mbalimbali na kuzichambua. Wajumbe wa kamati hiyo ni Dk. Marcellina Chijoriga, Profesa Ibrahim Juma, Mtesigwa Maugo, Dk. Mussa Assad na Dk. Hamisi Kibola. Katika ripoti hiyo iliyokabidhiwa, Profesa Mshoro alikabidhi vitabu viwili; kimoja kikiwa cha ripoti husika na kingine kikihusisha nyaraka mbalimbali walizoona ni muhimu ziendane na ripoti hiyo