Arsenal bado wanahitaji huduma ya Mudryk

Arsenal bado wanahitaji huduma ya Mudryk

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
ARSENAL BADO WANAKOMAA NA MUDRYK

RASMI: Klabu ya Arsenal imetuma ofa ya pili ya kumsajili nyota wa Shakhtar Mykhaylo Mudryk baada ya ile ya kwanza ya €40m na nyongeza ya €20m kukataliwa.

Kwa mujibu ripoti, Arsenal wametuma ofa ambayo wanaamini itamaliza dili hilo.

Ikumbukwe Shakhtar wanataka kiasi kisichopungua €55m bila kipengele cha nyongeza ya kulipa baadae kama atakuwa kwenye kiwango kikubwa akiwa na Arsenal.

Mazungumzo yanaendelea kati ya klabu zote mbili.
 
Jamaa yuko vzr aje2 itakuwa super sub, maana arsenal upande wa sub hayuko vzr.kwamfano sub ya saka na martinel waga ni kipengelee
 
Dogo yuko moto sana, ni zaidi ya Anthony wa Man Utd, na yule aliyeenda Barca alitoka Leeds Utd...

Mudryk ni bonge la winger..anavyopepea na zile nywele utampenda bure..
 
Back
Top Bottom