Arsenal for Everyone®, kampeni ya kuhamasisha ushoga na usagaji

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Wikiendi hii nilikuwa ubanda nikitazama mechi kati ya Yanga na Ndanda, hapo nilipokuwepo televisheni nyingine ilikuwa inarusha mchezo wa Arsenal na Newcastle.

Sikuwa na muda sana na mchezo huo (sio mtazamaji sana wa Soka la Ulaya siku hizi) lakini nilivutwa na kampeni iliyokuwa inaendelea kwenye mbao za matangazo za Uwanja wa Emirati.

Kampeni ilikuwa na maneno, 'Arsenal for Everyone' kisha kufuatiwa na mkururo wa rangi ambao unatambulisha makundi ya wasagaji, mashoga, wadau wa wapenzi ya tofauti na waliojibadili jinsi (LGBT).


Kufuatilia kwangu kukanifikisha katika tovuti ya klabu hii na nikaona huko kuwa hii ni kampeni ambayo imekuwepo tangu 2008 ambayo kupitia kwayo klabu hii ya London huunga mkono harakati za makundi haya na kusherekea uhuru wa kuchagua aina ya maisha ayatakayo mja.

Arsenal For Everyone | News Archive | News | Arsenal.com

Arsenal for Everyone | Community | The Club | Arsenal.com

Kipo pia kikundi cha washabiki mashoga wa timu hii ambao wanaungwa mkono na uongozi wa timu kama washabiki wengine ambacho kinajiita 'Gay Gooners'. Gay Gooners | Fans | Arsenal.com



Picha hapo juu inawaonesha washabiki wa Arsenal wakishiriki katika tamasha maarufu la kila mwaka la mashoga, wasagaji na wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja linalofahamika kama London Pride na picha hii na nyinginezo ziliwekwa katika tovuti rasmi ya Klabu ya Arsenal. Arsenal LGBT at London Pride | News Archive | News | Arsenal.com

Wachezaji wa Arsenal walishiriki katika kampeni maarufu ya kusapoti ushoga mchezoni inayoitwa 'Rainbow Laces' ambapo walipiga picha za video ya dakika moja inayoonesha wakivaa viatu vya mpira vyenye kamba zenye rangi za upinde wa mvua ambazo huwatambulisha mashoga na wasagaji.




[video]www.youtube.com/watch?v=1_2QzUvLNDI[/video]

Maoni yangu: Ni wakati wa watu (Waafrika) kutathimini tena ushabiki wao kwa vilabu vya Ulaya na soka lao ambao kwa muda mrefu umekuwa ukituumiza kiuchumi, ukididimiza soka letu na sasa unatupeleka kule ambako maadili yetu na ubinadamu wetu hautaki kuelekea.

Kwa muda nimepinga ufuasi wa soka la Ulaya kwa sababu za kiuchumi na ukweli kuwa tuna safari ya kurekebisha mchezo wetu na kufanya uchumi wa Soka ubaki kwetu Afrika kwa manufaa yetu. Sasa nina sababu nyingine nyingi za kiadili na kiroho za kutounga mkono ushabiki huu upofu!

Wasalaam!

Aione: Viper
 
Shabikia game safi inayochezwa na wachezaji wa Arsenal, hayo mengine waaachie wao!!
 
Angalia mpira, enjoi, yasiyokuhusu waachie wao, wenzetu dunia nyingine kule, wanaamini kila mtu ana uhuru na haki ya kuchagua kuwa au kufanya atakalo, cha muhimu asivunje sheria zao.
 
Kuwa mshabiki wa timu yoyote ya mpira ya ulaya au kwingineko haina maana unaunga mkono upumbavu mwingine unaondelea ndani ya timu hiyo kwa mfano hili la ushoga. Wapenzi na mashabiki mbalimbali duniani wanaozipenda timu hizo wanazipenda kwa kandanda pekee na si huu upumbavu mwingine ambao baadhi ya nchi duniani zinajitahidi mara kwa mara ili uungwe mkono na kila nchi duniani zikiwemo nchi za Kiafrika.

Shabikia game safi inayochezwa na wachezaji wa Arsenal, hayo mengine waaachie wao!!
 
Sizinga,
Hawa watu tunaowashabikia wana athari za kisaikolojia kwenye maisha yetu, hatuwezi kuepuka wanayoyafanya nje ya 'soka lao safi'. Huko ni kujitia upofu...
 
Last edited by a moderator:
truegooner, huwezi kuangalia burudani inayotolewa na watu wanaounga mkono ambavyo uko kinyume navyo. LAzima tukubali kuwa mtazamo wao una athari kwa ninyi washabiki wao, fikiria kama wangekuwa wanaunga mkono vitu vinavyokugusa zaidi, mauwaji kwa mfano. Bado ungesema tuangalie burudani tu?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…