Arsenal ijivue gamba!!

Arsenal ijivue gamba!!

samirnasri

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
1,388
Reaction score
213
Timu ya arsenal imetimia miaka sita (misimu sita) bila kuchukua kikombe chochote. Kwa takriba misimu minne iliyopita timu hiyo imekuwa ikianza na kasi ya ajabu na kuonesha dalili ya kuchukua ubingwa lakini wamekuwa wakichemsha katika mechi za mwishoni kiasi cha kutungiwa jina la utani kuwa arsn ni baskeli ya miti. Sasa ni wakati wa arsenal kujivua gamba ili izaliwe upya na kuanza upya msimu ujao baada ya leo kupoteza rasmi muelekeo.
 
Naam. Ni kweli kabisa. Kocha ni mzuri tu, ila SERA imeshindwa. Ni lazima kuingia sokoni kama wengine.
 
Bila usajili wa maana hata miaka 100 hawatachukua kombe,hata kocha ameishiwa mbinu,kunatakiwa mabadiliko makubwa hata kocha wamtimue,hana jipya.
 
Bila usajili wa maana hata miaka 100 hawatachukua kombe,hata kocha ameishiwa mbinu,kunatakiwa mabadiliko makubwa hata kocha wamtimue,hana jipya.

kuvunjika kwa pakacha.....,pilipili usiyokula....., maumivu ya kiatu ayajuaye mvaaji, adhabu ya kaburi aijuaye maiti, koti likikubana vua.arsen naona waenderee hivo ivo.
 
Sasa arsenal ikichukua ubingwa nani tutakuwa tunamtania?
 
kawaulize kwanza waliojivua magamba ni majoka au binadamu na wamepata maumivu gani.Kama ni nyoka dawa yake ni kumuu sio kuvua gamba.Kawaambie wazazi wa kolo ture,fabrigas,song and co.hiyo habari ya kuvua gamba kama hawajakuchoma kisu.!!!
Timu ya arsenal imetimia miaka sita (misimu sita) bila kuchukua kikombe chochote. Kwa takriba misimu minne iliyopita timu hiyo imekuwa ikianza na kasi ya ajabu na kuonesha dalili ya kuchukua ubingwa lakini wamekuwa wakichemsha katika mechi za mwishoni kiasi cha kutungiwa jina la utani kuwa arsn ni baskeli ya miti. Sasa ni wakati wa arsenal kujivua gamba ili izaliwe upya na kuanza upya msimu ujao baada ya leo kupoteza rasmi muelekeo.
 
Kolo toure mbona alihama arsenal siku nyingi sana.
 
Arsenal kama betri linaanza kwa speed kubwa jinsi linavyo2mika ndio linazidi kuisha.
 
Back
Top Bottom