Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Suarez alikuwa hafurahii maisha ndani Anfield 2013 na alikuwa anataka kuondoka. Liverpool walimuambia hawana shida, wapo tayari kufanya mazungumzo na klabu yoyote aliyopo tayari kujiunga nayo.
Arsenal wakiwa wametangaza nia kweli ya kumsajili Suarez walituma ofa Liverpool ya kumsajili Suarez. Suarez alikuwa tayari kujiunga na Arsenal.
Arsenal waligundua kwenye mkataba wa Suarez kipo kipengele kinachoitaka klabu inayotaka kumsajili kulipa zaidi paundi 40 milioni. Wakatuma ofa ya paundi 40 milioni kwa Liverpool.
Liverpool wakawarudisha wakiwataka wafike kigezo cha mkataba ambacho kinawataka kulipa zaidi ya paundi 40 milioni.
Arsenal wakarudi, wakaa chini wakajadili halafu wakatuma ofa ya paundi milioni 40+1. Nielewe vizuri, hawakuongeza paundi milioni moja bali paundi moja. Yaani 2500 za kitanzania[emoji3].
Ndipo mmiliki wa Liverpool John Henry, alikasirika na kwenda Twitter kuwadhihaki Arsenal. Kupitia ukurasa wake wa Twitter aliweka picha ya Suarez na kuandika.
“What do you think they’re smoking over there at Emirates?”
Kwa kindereko kisicho rasmi ni kuwa "Unafikiri wanavuta nini huko Emirates?"
Lakini kweli Arsenal walikuwa wanavuta jani la wapi?? Yaani unaambiwa ukaongeze hela ya kumsajili Suarez halafu unaongeza shilingi elfu mbili kweli? Ila haishangazi hawa ni Arsenal[emoji1783].
Msimu mmoja mbele, Barcelona walilipa zaidi ya paundi 70 milioni kumsajili Suarez. Ni karibia mara mbili ya dau waliloliweka Arsenal mwaka mmoja nyuma.
[emoji871]@deo_mwanasoka