Arsenal kushinda Ubingwa wa EPL halikuwa lengo mama hivyo lawama pelekeni kwenye timu zenu

Anigrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
1,680
Reaction score
4,204
Kumekuwa na ibuko la Threads nyingi zikiongelea Arsenal na kuiombea mabaya kutokana na mwendelezo wake katika ligi kuu ya England (EPL).

Mashabiki wengi wa Team pinzani kama vile Man u, Chelsea na baadhi ya Liverpool mixer na Man city.

Sasa jamani naona mipasho imekuwa mingi sana kwa Arsenal, ohhh hawafiki popote,hawawezi kuchukua ligi,ohhh hawajakutana na Team Bora, ohhh wakipata majeruhi kidogo tu hawamalizi ata nafasi ya 4.

Jamani lawama pelekeni kwenye Team zenu, kuna team nyingi ambazo mwanzo zilionesha kuwa zinalitaka kombe la EPL kuliko Arsenal na hiyo ilikuwa wazi kutokana na sajiri zao.

Sasa kama Man u, Chelsea, Totenham,Man city na Liverpool zimesajiri sajiri kubwa zaidi ya Arsenal iweje leo Ng'eng'eng'e ziende Kwa Arsenal na sio kwenye Team zenu?

Malengo ya Arsenal msimu huu ilikuwa ni kushiriki mashindano ya UEFA ili iweze kushawish baadhi ya wachezaji kujiunga nao ila kushawishi wachezaji wao wazuri wabaki.

Kitendo cha Arsenal hadi sasa kukaa pale juu ni Over achieve...! Arsenal wapo juu kutokana madhaifu ya Team zenu sasa iweje manung'uniko yenu mnayaelekeza kwa Arsenal?

ata kama Arsenal atamaliza nafasi ya 2 bado kwake ni mafanikio makubwa kwani ubingwa haukuwa lengo, ila kutokana na ujinga wa team zenu ndomana Arsenal yupo hapo juu.

Kuna Team imesajili mabeki wengi wa bei mbaya utadhani inacheza Rugby ila hadi sasa imefungwa magoli mengi kuliko mechi ilizocheza ila hadi sasa ni vimbembele kuisema Arsenal.

Kuna Team imepigwa hela ndefu Kwa Winger ambae hadi leo ana goli 3 tu ila mbwembwe utadhani Kisinda, ila wenye mchezaji wao kutwa kuifungulia nyuzi Arsenal.

Narudia tena wenye Arsenal yetu lengo ni kushiriki Champions league ila kama ikitokea tumechukua ubingwa sie tutampa atakaemaliza nafasi ya 2, Kwahiyo nyie mliosajiri ili muwe mabingwa pambaneni sana ili mmalize nafasi ya 1 au ya 2.
 
Kama washindani wao Man City, Spurs na Chelsea kila wiki wanayakanyaga, hakuna kitakachomzuia
 
Chelsea katumia €400m kuanzia summer had sasa January na anaweza kufika €500m

Man u wametumia €250m

Westham katumia €183m

Wolves, Spurs & Forest wametumia over €150m

Arsenal tumetumia €125m tu , Sasa lawama pelekeni kwenye Timu zenu kwa sajili mbovu
 
Waambie hao kaka. Wanazi wa arsenal tumechoka na ujinga wao mitaani na mitandaoni
 
Waambie hao kaka. Wanazi wa arsenal tumechoka na ujinga wao mitaani na mitan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…