MILL8
JF-Expert Member
- Aug 27, 2015
- 1,837
- 879
AMA kweli maisha bila unafiki hayaendi. ndicho unaweza kusema kuhusu Aserne Wenger baada ya mashabiki wa timu hio jumapili aprili 22 kubeba mabango ya kumpongeza kocha huyo siku chache tu baada ya kutangaza kwamba ataachia ngazi mwisho wa msimu. tofauti na ilvyozoeleka siku za karibuni ambapo mashabiki hao walikuwa wanabeba mabango ya 'wenger out', jumapili hio mambo yalikuwa tofauti huko emirates wakati wenger alipokiongoza kikosi chake kwa mara ya kwanza tangu alipotoa kauli hio. Arsenal ilicheza na West Ham United na kushinda 4-1 kwenye mchezo wa ligi kuu, huku straika Alexandre Lacazetteakipiga mbili.kati mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki 59,422.