Arsenal imefanikiwa kuwa namba moja katika Premier League baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Brighton huku Aston Villa ambayo nayo imekuwa na msimu mzuri ikishika nafasi ya pili kwa kuifunga Brentford magoli 2-1.
Arsenal imefikisha pointi 39, Aston Villa ikiwa na 38, zote zikiwa zimecheza mechi 17.