Arsene Wenger kuacha kuinoa Klabu ya Arsenal mwisho wa Msimu huu 2017/18

Arsene Wenger kuacha kuinoa Klabu ya Arsenal mwisho wa Msimu huu 2017/18

abudist

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2009
Posts
850
Reaction score
781
Arsene Wenger: Arsenal meneja ataondoka klabuni baada ya miaka 22 kama meneja. Amewashukuru wapenzi wa soka wa klabu hiyo kwa kumpa heshima na ushirikiano miaka hiyo yote. Wenger, 68, kashinda Premier League mara 3 na FA Cups mara 7, pamoja na Double mwaka 1998 na 2002.

=========

nankumene said Mkufunzi Arsene Wenger anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu hatua inayokamilisha uongozi wake miaka 22 katika klabu hiyo.

Raia huyo wa Ufaransa anaondoka mwaka mmoja kabla ya kandarasi yake ya miaka miwili kukamilika,

Arsenal iko katika nafasi ya sita katika ligi ya Uingereza na inatarajiwa kukosa katika nafasi nne bora kwa msimu wa pili mfululizo huku matumaini yao ya kushiriki katika fainali za kombe la vilabu bingwa Ualya yakitegemea iwapo watashinda kombe la ligi ya Yuropa.

Wenger mwenye umri wa miaka 68 alishinda mataji matatu ya ligi ya Uingereza na mataji manne ya kombe la FA ikiwemo makombe yote mawili mwaka 1989 na 2002

''Nashukuru kwa kupata fursa ya kuhudumia klabu hii kwa muda mrefu'', alisema Wenger.

''Nimeiongoza klabu hii vizuri kwa kujitolea na maadili mema. Kwa mashabiki wote wa Arsenal , tunzeni maadili ya klabu hii''.

Arsenal imesema kuwa mrithi wake atatangazwa haraka iwezekanavyo.

Mmiliki wa Arsenal na mwanahisa mkuu Stan Kroenke alielezea tangazo hilo la siku ya Ijumaa kuwa ni mojawapo ya siku ngumu zaidi katika miaka yote ya mchezo wa soka.

Aliongezea: Sababu kuu ya sisi kushirikiana na Arsenal ilikuwa kutokana na kile kilicholetwa na Arsene Wenger ndani na nje ya uwanja. Uongozi wake wa muda mrefu na ukufunzi mzuri hauwezi kamwe kuafikiwa na mtu yeyeto.

_100954503_wengerplstats.png

Raia huyo wa Marekani aliisifu rekodi nzuri ya Wenger akiongezea kuwa aliubadilisha mchezo wa klabu ya Arsenal na soka ya Uingereza kupitia maono yake kuhusu vile soka inavyoweza kusakatwa.

Baada ya kuajiriwa tarehe 1 mwezi Oktoba 1996, ndio meneja wa ligi ya Uingereza ambaye amehudumu kwa muda mrefu na amesimamia rekodi ya mechi 823.

Lakini mashabiki wengine wamekasirishwa na raia huyo wa Ufaransa katika misimu miwili iliopita kutokana na mchezo wao katika ligi.

Kupoteza kwa 2-1 dhidi ya Newcastle ilikuwa ya 11 katika ligi msimu huu ikiwa ni rekodi mbaya zaidi chini ya usimamizi wake, wako nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City kwa kwa pointi 33 na pointi 33 juu ya Klabu ya Westbrom ilio chini ya jedwali ikiwa na pointi 21.

Arsenal ilimaliza nje ya timu nne bora kwa mara ya kwanza tangu Wenger awasili katika klabu hiyo na sasa wako pointi 14 nyuma ya timu iliopo katika nafasi ya nne katika jedwali la ligi Tottenham hotspurs ikiwa zimesalia mechi tano kuchezwa.

Watakabiliana na klabu ya Uhispania Atletico Madrid ambao wako katika nafasi ya pili katika ligi ya La Liga, katika nusu fainali ya kombe la Yuropa huku awamu ya kwanza ya mechi ikitarajiwa kuchezwa Alhamisi ijayo.

_100960687_299efa99-24c6-4f2c-a43d-f8ca16237cec.jpg

Image captionAlan Shearer anasema kuwa wachezaji wa Arsenal hawafanyi wanachotakiwa kufanya na Wenger
Matatizo yaliomkumba Wenger
Wenger alishinda mataji matatu ya ligi ya Uingereza na makombe manne ya FA katika misimu yake tisa ya akwanza akiwa mkufunzi.

Mwaka 2003-04, alikuwa mkufunzi wa kwanza tangu 1888-89 kuongoza timu ya Uingereza bila kufungwa msimu mzima .baada ya kushinda kombe la FA 2005, walisubiri miaka mingine tisa ama siku 3,283 kujipatia taji jingine . hatimaye walifanikiwa kwa kuishinda Hull City ili kuweza kushinda kombe la FA 2014kabla ya kushinda tena kombe hilo msimu uliofuatia.Kwa kuishinda Chelsea 2-1 katika uwanja wa Wembley, lakini ikamaliza pointi 18 nyuma ya kikosi cha Antonio Conte

Timu yake imeshindwa kufurukuta Ulaya tangu iliposhindwa na Barcelona katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya 2006.

Walibanduliwa katika mondoano wa kufuza robo fainali kwa msimu wa sita mfululizo huku wakishiriki katika taji hilo 2017 mara ya mwisho na kupoteza 10-2 kwa jumla dhidi ya Bareyn Munich.

Mwaka 2006, walihamia katika uwanja wa Emirates uliogharimu £390m baada ya kuondoka Highbury

Arsenal imekuwa ikitumia fedha kidogo ikilinganishwa na wapinzani wao katika ligi ya Uingereza kuhusu usajili wa wachezaji. Lakini Wenger alivunja rekodi ya klabu hiyo mara mbili msimu huu.

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette alijiunga na klabu hiyo katika dirisha la uhamisho kwa dau la £46.5m, huku mchezaji wake wa mwisho aliyemsajili akiwa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang aliyegharimu £56m mwezi Januari.

_100960686_3fd5aaa4-2a3b-40d0-b6e2-a27868d5ced4.jpg

Image captionArsenal iliposhinda kombe la FA dhidi ya Chelsea 2017
Ni nani atakayemrithi?
Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel tayari amehusishwa na kazi yake huku Wenger akisema kuwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Patrick Viera ana uwezo wa kumrithi.

Tuchel anapigiwa debe na wachanganuzi kwa sasa mbele ya mkufunzi wa Ujerumani Joachim Low na mkufunzi wa zamani wa Real Madrid, AC Milan na Chelsea Carlo Ancelotti.

"Tuna malengo ya kuijenga Arsenal na kuhakikisha kuwa inashinda mataji mengi katika soka'', aliongezea Kroenke

Chanzo: BBC Swahili
 
Arsene Wenger is to leave Arsenal at the end of the season, ending a near 22-year reign at the club.

The Frenchman departs a year before his latest contract was due to expire.

The Gunners are sixth in the league and set to miss out on a top-four spot for the second straight season, with their hopes of reaching the Champions League resting on winning the Europa League.

Wenger, 68, won three Premier League titles and seven FA Cups, including the Double in 1998 and 2002.

"I am grateful for having had the privilege to serve the club for so many memorable years," said Wenger. "I managed the club with full commitment and integrity.

"To all the Arsenal lovers, take care of the values of the club."

Arsenal majority shareholder Stan Kroenke described Friday's announcement as "one of the most difficult days we have ever had in all our years in sport".

He added: "One of the main reasons we got involved with Arsenal was because of what Arsene has brought to the club on and off the pitch.

"His longevity and consistency over such a sustained period at the highest level of the game will never be matched."

Appointed on 1 October 1996, he is the Premier League's current longest-serving manager and has taken charge of a record 823 games.

But some fans have turned on the Frenchman over the past two seasons as a result of their league performances.

Sunday's 2-1 defeat at Newcastle was their 11th in the league this season, equalling their worst tally in a campaign under Wenger.

They are 33 points behind leaders Manchester City, who have 87 points, and the same number away from bottom side West Brom, who have 21.

Arsenal finished outside the top four last term for the first time since Wenger arrived at the club, and are now 14 points behind fourth-placed Tottenham, with five matches remaining.

They face Spanish side Atletico Madrid, who are second in La Liga, in the Europa League semi-finals, with the first leg on Thursday.
 
OOOHH HALELUYAH naoa ukombozi unatua Arsenal.Nimeiona hii babari mida hii skynews Wenger kaongea mwenyewe,ngoja nijiandae kurudi kuishangilia timu yangu,huyu mzee mm alinipa likizo ya kutoishangilia Arsenal.
 
Arsene Wenger: Arsenal meneja ataondoka klabuni baada ya miaka 22 kama meneja. Amewashukuru wapenzi wa soka wa klabu hiyo kwa kumpa heshima na ushirikiano miaka hiyo yote. Wenger, 68, kashinda Premier League mara 3 na FA Cups mara 7, pamoja na Double mwaka 1998 na 2002.
Good news!
 
HII NEWS ITAFUNIKA KIKI YA NDOA YA KIBAKULI, I THINK
 
Daaah so sad, why lakini? Please Wenger stay wewe ni kocha bora. [HASHTAG]#bringbackourWenger[/HASHTAG]
 
OOOHH HALELUYAH naoa ukombozi unatua Arsenal.Nimeiona hii babari mida hii skynews Wenger kaongea mwenyewe,ngoja nijiandae kurudi kuishangilia timu yangu,huyu mzee mm alinipa likizo ya kutoishangilia Arsenal.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] anatania tu man. Bado yupo yupo sana
 
Ngoja msimu uishe kwanza, akishaondoka na akaja kocha mwingine ndio nitaamini.
 
Mimi mpaka siku nisimuone kwenye benchi la ufundi.. Vinginevyo huyo mzee anavoaminiwa na bodi lolote lawezakuwa ikiwepo kusalia hapo klabuni
 
Huyu mzee ndiyo aliyenifanya niuchukie mpira total, huyu wenger anaweza akaja kuwa remote cotrol ya huyo kocha mpya...
 
it is official, he will step down at the end of the season. Wamiliki imebidi kufanya hivyo kwa sababu mashabiki walianza kususia kuja uwanjani. Kama wewe ni mfuatiliaji wa mpira, many seats were empty.
tuta-mmmiss
 
Brendan Rodgers is loading..................
 
Daaah so sad, why lakini? Please Wenger stay wewe ni kocha bora. [HASHTAG]#bringbackourWenger[/HASHTAG]
Maboso kule nyanda za juu kusini ni uchafu unaobaki toka kwenye pombe inaitwa ulanzi, na comment yako Naona ni maboso pure
 
Back
Top Bottom