Artificial Intelligence platforms

1. ChatGPT - Ni tool ya mazungumzo inayotumia teknolojia ya artificial intelligence (AI) kutoa majibu, msaada, na ufafanuzi kwa maswali mbali mbali. ChatGPT inaweza kukusaidia juu ya maswala ya elimu, kujifunza kutumia programu za kompyuta, ushauri wa kibiashara, au hata kujibu maswali ya kila siku. Inapatikana Playstore/Appstore/Microsoft Store na unaweza ukatumia kwenye browser yako kama unaona ni changamoto kuwa na apps nyingi kwenye device yako.

Unaweza kuuliza chochote kile na ikawa ina msaada wa kukupa majibu.
 
2. Ideogram Ai - ni teknolojia inayotumia akili bandia (AI) kutengeneza picha na michoro kwa kutumia maelezo au maagizo ya maandishi. Inatumia njia ya kisasa ya kuunda michoro na picha kwa kutumia maelezo ya maandishi pekee, na inaweza kutumika katika nyanja mbalimbali kama vile ufanisi wa sanaa, uundaji wa michoro ya ubunifu, na hata kufanya product development. Teknolojia hii ni sehemu ya mageuzi yanayoongezeka katika uwanja wa sanaa ya dijitali na inachangia kubadilisha jinsi watu wanavyojieleza kwa kutumia picha na michoro.

Hii inaweza kukusaidia kurahisisha kutengeneza posters, logos, flyers, infographics, mockup na vitu vingine vingi kwa kuielezea dhamira yako, rangi na viti vingine. Hii ni nzuri sana ukiwa unajua chochote kuhusu graphics designing, lakini pia kama hufahamu chochote inaweza kuwa chanzo cha kukupa majibu ya kazi unayoitaka, labda unayaka logo lakini huitaji kuzunguka sana kutumia graphics designer, basi unaiomba ikutengenezee logo unayoitaka kisha graphics designer ataweza kukupa ile yenye ubora wa hali ya juu.
 
Chatgpt inafanya mambo mengi sana. Hadi logo inatengeneza. Lakini bado ina mapungufu, mfano kupata logo kwa viwango na taste uzitakazo inafail. Naikubali sana kwenye Augmentation ya documents. Niliipa document ikanifanyia analysis ndani ya dakika 1.
 
Deepseek unlocked
Deepseek Ai ni bora pia kwa sababu inaweza kukupa majibu bure, kukupa picha bure na baadhi ya sifa nyingi sana ,na inatumia language model ya R1 ,ila changamoto yake ni kuwa inaelemewa kila wakati kiasi cha kufanya watumiaji tusipate majibu kwa wakati
 
Chatgpt inafanya mambo mengi sana. Hadi logo inatengeneza. Lakini bado ina mapungufu, mfano kupata logo kwa viwango na taste uzitakazo inafail. Naikubali sana kwenye Augmentation ya documents. Niliipa document ikanifanyia analysis ndani ya dakika 1.
Tumia Ideogram Ai
 
03. Venngage Ai - Hii ni teknolojia inayotumika kutengeneza inforgraphics kwa ajili yako wewe mwenyewe, kampuni au taasisi.

Hii hauna haja ya kuandika mambo mengi sana, naweza kuifananisha na Canva, unachukua template tu kisha unapachika then boom kinatokea kitu ubaweza uka-submit kwenda kwa mhusika au kuitumia wewe mwenyewe.
 
Ina app yake na vipi Matumizi yake haswa inadeal na nini na utofauti wake na AI nyingine ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…