Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,468
- 2,349
Mara ya kwanza kuingia katika mji wa Arusha ilikuwa ni mwaka 1977, nikitokea mji wa Dodoma, kwa njia ya barabara. Safari hiyo ilichukua jumla ya masaa nane. Nilifika Arusha mjini usiku wa saa mbili. Tulipokfika Ngarenaro mji ulikuwa umajaa taa za mafuta, ukimulika giza la mji huu, kupita dirisha la gari niliokuwemo niliweza kuona mizunguko ya watu katika eneo hilo, wengi wao wakiwa ni wanaume. Niliweza kuona biashara kadhaa kando kando ya barabara kati ya hizo ikiwa ni mishikaki.
Hata tulipofika Uhuru road(Sokoine road), Nyumba za mbafu za mbwa zilifika kikomo, hapo niliweza kuona maduka makubwa kabisa, duka la kwanza kulitia machoni lilikuwa ni RTC, pembeni yake kulikuwa na kituo cha mafuta na nyuma yake kulikuwa na kituo cha treni.
Gari lilizidi kusonga mbele, huku nikishangaa mataa barabarani, Uhuru road ilikuwa tofauti sana na mtaa wowote niliowahi ku'uona Dodoma, hadi tulipofika mnara wa saa, nilitamani kurudi tena na kuangalia barabara ya uhuru! Dereva alizungusha gari na kuingia New Arusha Hotel.
New Arusha hotel ilikuwa ni tofauti sana na hoteli za Dodoma, kuanzia majengo yake hadi huduma zake. Hapa nina maana ya Dodoma Hotel, kwani ndio ilikuwa hotel kubwa kabisa wakati huo. Sijui sasa kuna hotel gani kubwa hapo Dodoma. Gari liliposimama wahudumu wawili walikuja kutulaki na kusaidia kubeba mizigo yetu. Kumbuka kuwa sikuwa peke yangu!
Baada ya kukamilisha taratibu za usajili, wahudumu wale walituzogeza kwenye korido, na kubonyeza kitufe kwenye ukuta, mara pakafunguka! wakaingia ndani huku wakituharishia tuwafuate, roho ilisita, macho yakanitoka! Hawa wahudumu wanataka kunipeleka wapi? Wezangu sijui kama walikuwa na mawazo kama yangu, kwani wailingia moja kwa moja kwenye kichumba hiko. Baada ya kufikili kwa sekunde kadhaa nami niliingia. Mlango ukajifunga na mhudumu kabonyeza namba tatu... Sikujua awali kuwa ile ilikuwa ni lift!
Tulikaa hotelini hapo kwa siku saba, nikawa mwenyeji na nikipanda lift zaidi ya mara kumi kwa siku, kiasi cha kuwakera baadhi ya wahudumu wa hoteli.
Makaazi mpya yalikuwa ni katika eneo E, ni eneo la viwanda. Ila eneo hilo lilikuwa linakaliwa na watu wengi ambao walikuwa wakifanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Sio mtaalamu sana wa mipango miji, ila ndio hivyo, nyumba ziikuwa zimepakana na kiwanda cha bia na kiwanda cha sabuni na peremende.
Hata baada ya siku kadhaa hapo mtaani, nilijua kumbe kuna viwanda vingi zaidi, kama kiwanda cha biskuti, kiwanda cha kiko na kiwanda cha nguo(Kilitex).
Ilikuwa ni shida kubwa kwenda dukani, maduka ya karibu yalikuwa yapo Sinoni, na ni baada ya kuvuka mto Themi(temi), Kuvuka mto huo inakubidi kutumia njia ya treni(reli). Kipindi hiki kilikuwa maarufu kwa mikate ilyojulikana kama kisu, ambayo uliweza kuinunua mzima ama nusu na hata robo yake. Maduka mengine yalikuwa ni Kijenge.
Shule za msingi nazo zilikuwa ni mbali, aidha hazikuwa nyingi hivyo, nakumbuka kuilkuwa na shule ya msingi Naura, Meru na Uhuru aidha na ile ya kiingereza Arusha School. Hizi ndizo zilikuwa za karibu. Kama mwanafunzi ama mwalimu mwendo ulikuwa ni wa miguu!
Zaidi huduma nyingi zilipatikana mjini, na hapakuwepo na daladala ama viford(nasikia siku vimejaa tele). Hivyo kwa mtu wa kawaida iimpasa kutembea kwa miguu kufika mjini. Hata hivyo kulikuwa na njia za mkato(shortcut) nyingi tu.
Burudani hazikuwa haba, Arusha ilikuwa na majumba mawili ya sinema, yakijulikana kama Metropol na Elite.. Metropol lilikuwa maarufu kwa aina ya simena walizokuwa wakionyesha nyingi zikitoka Ulaya na Marekani, aidha za Hong Kong na India, Jumba lao lilikuwa zuri na tofauti sana na lile ya Elite Cinema. Elite waliweza kuwakusanya wanafunzi wengi waliokuwa wakipenda kutoroka shule kwani katika siku za kazi waiweza kufungua jumba lao tokea saa nne asubuhi, huku Metropol wakianza saa kumi na mbili jioni.
Kulikuwa na sehemu za kuogelea kama pale New Arusha Hotel, Mount Meru Hotel na katika shule ya Arusha, aidha bembea za watoto zilikuwepo kuanzia Gymkhana hadi New Arusha Hotel. Viwanja vya gofu vikiwa Gymkhana na Mount Meru hotel.
Pale Sheikh Amir Abeid, tuliweza kushuhudia mashindano mbalimbali, kilichovutia miaka hiyo ni mashindano ya riadha... Yalivutia wengi na hasa vijana. nakumbuka ukiondoa mashindano ya Afrika Mashariki, wanafunzi wengi walikuwa wakicheza hapo na hasa siku za mwisho wa wiki huku washindi wakizawadiwa Zabibu za Dodoma.
Ukizungumzia michezo basi hutowacha kuangalia jinsi shule ya Arusha(Arusha school) na ile ya St Constantine walivyoweza kuwa na aina nyingi sana za michezo. Walikuwa na rugby, Kriket, michezo ya Farasi na hii mingine ya kawaida. Siku ukisikia kuwa katika shule hizo kuna open door kwa michezo, hakuna aliyependa kukosa.
Shule za msingi nazo zilikuwa na vituko kibao, kwa mfano shule ya Naura ilikuwa siku zote ikipigana na shule ya Meru, hata hivyo shule ya Uhuru ndio iliyokuwa na wababe kibao, kuanzia akina babu wa Kale na kundi lake... Hawa waliweza kutawala shule zote za mjini Arusha.
Nchi iliingia vitani, na baada ya vita vya Kagera, pale mtaani palibadilika sana. Watu walikuwa ni wengi mno karibu na milango ya viwanda. Awali nilizoea kuwanona vibarua, lakini sasa hawakuwa tena vibarua, bali ni wafanya magendo.
Huwezi kuamini kuwa bia ilikuwa inatowela kiwandani katika ndoo, na kukabidhiwa kwa wanamagendo. Upande wa kiwanda cha sabuni (EMCO) hizi zilikuwa zikivushwa kwa wingi kupitia kwenye fence ya kiwanda hicho. Lawalawa aka peremende hazikuwa na soko la kimagendo kwani tayali kulikuwa na ubani kwa jina la Big G toka Kenya.
Kwenye kiwanda cha biskuti, hali ilikuwa njema ukiondoa tatizo la watoto kujazana tele kwenye jaa la kiwanda hicho ili tu kupata kuokota biskuti zilizotupwa toka kiwandani hapo. Kwa kipindi hicho tabia hii ya watoto kujazana kwenye jaa la kiwanda na hasa siku za mwisho wa wiki halikuwa likitoa picha yoyote zaidi ya kwamba watoto wanavutiwa zaidi na harufu nzuri ya biskuti. Iwapo kiwanda hiki kama kipo hadi leo basi jaa lao litakuwa ni sehemu ya homeless na street children.
Magendo haya yalikuwa ni ya wazi, tokea viwandani hadi mipakani. Kuanzia mirungi hadi dawa za meno kutoka Kenya. Mji ulichangamka na wengi wakanawili. Arusha ikiwa ni Arusha kwelikweli, kila kitu kikipatikana...
Mwaka 1983 niliondoka katika mji huu, ambapo tayali vita dhidi ya uhujumu uchumi ikiwa imeanza...