Arusha: Akutwa amefariki nyumbani kwake baada ya kutoka msibani huku mwili wake ukitokwa damu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Silasi Ndosi (38) mkazi wa Shangarai wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha amekutwa amefariki dunia, huku mwili wake ukiwa na majeraha ya mikwaruzo sehemu za kifuani na mgongoni.

Mbali na mikwaruzo pia mwili huo ulikutwa ukitoka damu puani, masikio, na mdomoni.

Akizungumza leo Novemba 14, 2024 kuhusu kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema kuwa mwili wa Ndosi ulibainika alfajiri ya Novemba 12, 2024 huko nyumbani kwake Shangarai iliyoko wilayani Arumeru.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Mount Meru kwa uchunguzi zaidi kujua chanzo cha kifo chake huku upelelezi ukiendelea,” amesema Kamanda Masejo.

Kaka wa marehemu, Elibariki Ndosi amesema kuwa aligundua mdogo wake amefariki alfajiri wa saa 12 asubuhi wakati alipokwenda nyumbani kwake.

“Tulikuwa naye jana hadi saa tano usiku kwenye msiba wa jirani ambapo tulishiriki shughuli zote za msiba kuanzia kuchimba kaburi hadi kumsitiri jirani yetu na akaenda nyumbani kwake kulala akiwa mzima wa afya,” amesema.
Screenshot 2024-11-14 101202.png

Chanzo: Mwananchi
 
Siri ya kaburi aijuaye maiti, hata ndugu wa marehemu hawajui alikutwa na nini hadi kupatwa na majeraha hayo ya mikwaruzo kifuani na mgongoni hadi kufikwa na umauti.

Apumzike kwa amani.
 
Kifo ni kifo tu... Kauli mbiu ya banana Republic
 
Nahisi aliparamiwa na chombo cha usafiri akaamua kwenda kulala akidhani ni majeraha ya kupona yenyewe tu kumbe aliumia ndani kwa ndani.

Hasa madereva toyo wakikugonga na wakaweza kukimbia wanakimbia.

Nimeshashuhudia ajali kama mbili mtu anagongwa na toyo alafu toyo anakimbia au anamalizana kishkaji na mhusika kila mtu anaenda na hamsini zake.... Sasa ikiwa huyu aliparamiwa usiku huo huenda aliona ngoja akalale ili aone ataamkaje kesho yake
 
Siri ya kaburi aijuaye maiti, hata ndugu wa marehemu hawajui alikutwa na nini hadi kupatwa na majeraha hayo ya mikwaruzo kifuani na mgongoni hadi kufikwa na umauti.

Apumzike kwa amani.
Na sijui amekutwa nje au ndani maana habari za siku hizi huwa zinatuacha hewani
 
Silasi Ndosi (38) mkazi wa Shangarai wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha amekutwa amefariki dunia, huku mwili wake ukiwa na majeraha ya mikwaruzo sehemu za kifuani na mgongoni.

Mbali na mikwaruzo pia mwili huo ulikutwa ukitoka damu puani, masikio, na mdomoni.

Akizungumza leo Novemba 14, 2024 kuhusu kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema kuwa mwili wa Ndosi ulibainika alfajiri ya Novemba 12, 2024 huko nyumbani kwake Shangarai iliyoko wilayani Arumeru.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Mount Meru kwa uchunguzi zaidi kujua chanzo cha kifo chake huku upelelezi ukiendelea,” amesema Kamanda Masejo.

Kaka wa marehemu, Elibariki Ndosi amesema kuwa aligundua mdogo wake amefariki alfajiri wa saa 12 asubuhi wakati alipokwenda nyumbani kwake.

“Tulikuwa naye jana hadi saa tano usiku kwenye msiba wa jirani ambapo tulishiriki shughuli zote za msiba kuanzia kuchimba kaburi hadi kumsitiri jirani yetu na akaenda nyumbani kwake kulala akiwa mzima wa afya,” amesema.
View attachment 3151893
Chanzo: Mwananchi
Okay.

Homicide? Assassination? Poisoning attack?
Where specifically the scene of crime? Inside of the house or outside of the house in his homestead??
Alikuwa anajishughulisha na shughuli gani hasa? Alikuwa na ugomvi au Mgogoro na mtu yoyote yule?
Mawasiliano yake ya mwisho ya kwenye simu au mikutano ya face to face alikuwa na nani? Hali yake ya mahusiano ilikuwaje? Mwenza wake? Marafiki zake wa karibu? Mahusiano na wanafamilia wake yapoje? Kuna Mgogoro wa masuala ya biashara, Mali, mirathi au urithi kwenye familia yao ??
 
Ayubu 14: 1
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.

Pole kwa wafiwa.. maana unakufa hata chanzo nacho hakijuliani! Yampatayo mwanadamu kuna muda ni ngumu kueleza mana kuna muda kuna mambo yanatutokea ya hatari mpaka unawaza hapa nikifa nani atajua
 
Back
Top Bottom