Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Katika hali iliyotafsiriwa kama kuhakikisha Mahusiano mazuri na Makundi yote ya Kijamii, Chadema imekutana na Mashehe Jijini Arusha na kufanya nao mazungumzo, Yaliyofuatiwa na Dua kabambe.
Zaidi Taarifa kamili hii hapa
Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, Mhe. John Heche, akiwa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Bara, Mhe: Amani Golugwa, pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Mhe. Adv. Samwel Welwel, leo Ijumaa, Februari 21, 2025, wamekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Taasisi ya Twariqatul Qadiriyyat Arraziqyyat katika Makao Makuu yake, Zawia Kuu, iliyopo Kata ya Ngarenaro, Arusha.
Viongozi hao walipofika katika Makao Makuu ya Zawia Kuu, walipokelewa na viongozi wa Taasisi ya hiyo ambapo walifanyiwa dua maalum. Dua hiyo iliongozwa na viongozi wa taasisi hiyo, ikiwa ni ishara ya kuombea mafanikio, umoja na amani kwa chama na nchi kwa ujumla.
Viongozi wa taasisi hiyo walielezea furaha yao kuwa na viongozi hawa wakiwemo katika mazingira ya kiroho, wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano na maombi kwa ajili ya ustawi wa nchi na jamii.