Vipi hizo nzito hazifai kujengewa na gharama yake ni kiasi gani?
Tofali Nzito kwa bei ni tsh 1500 na ile nyepesi ni 750/
isipokua kujengea tofali nzito unatakiwa uimarishe msingi wa nyumba kwa ajili ya kubeba mzigo mzito maana tofali moja uzito wake ni 45-50kgs,
JIJI la Arusha na mitaa yake kuna ukosefu wa matofali mepesi ya block ya kujengea kutokana na mgodi wa kutoa material ya kutengeneza matofali hayo kufungwa na haijulikani lini utafunguliwa,
Yanayopatikana Ni yale matofali mazito ambayo hayatumiwi sana na wananchi wengi kutokana na gharama yake kua juu.
Elerai na Kerai ni nouma! Tofali zinamwagwa kutoka kwenye mende ka mawe!!!!!!!!!!!!
Msaada wa tafsiri aliyemwelewa Prince Hope anasema nini au anamanisha kitu gani?
Anamaanisha Matofali ya kerai hua ni imara sana hua hawashushi mojamoja wakifa site gari linabinua kama linamwaga mchanga au mawe na hakuna tofali linalovunjika.