Uchaguzi 2020 Arusha, Karatu: Tundu Lissu aendelea na mkutano wa kampeni viwanja vya mnadani

Uchaguzi 2020 Arusha, Karatu: Tundu Lissu aendelea na mkutano wa kampeni viwanja vya mnadani

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mkutano Mkubwa wa kampeni Mheshimiwa Tundu Lissu kwenye viwanja vya Mnadani Karatu Jimbo la Karatu - Arusha

Akiwa Karatu ametolea Ufafanuzi swala la mgombea ubunge jimbo la Karatu kupewa barua yakuitwa kwenye kamati ya maadili kwa kuzidisha mda wa mkutano, wakati mkutano sio wa mbunge. Amemuelekeza kuwa hamjibu mtu wa tume kuwa Mkutano haukuwa wa kwake.

Karatu sina chakuwaambia, hili ndo jimbo toka mwaka 1995 CCM hawana chao, nyie ndo walimu wa Demokrasia ya vyama vingi. Mmekuwa mkiifundisha Tanzania Nini maana ya demokrasia.

Sasa Karatu kitu chakuzingatia kwa siku zilizobakia Ni kuhakikisha tunakuwa na mawakala kwenye vituo vyote, mawakala wakuu na mawakala waakiba. Hakikisheni Mawakala wanaapishwa na wanaingia kwenye vyumba vya kupigia kura, na wakiingia hakikisheni mawakala wanapatiwa formu za matokeo. Fomu za Matokeo Ndo Ushahidi wa Matokeo kwenye kituo. Na Mwisho mkijihakikishia mmeshinda ingieni mtaani mkaijulishe Dunia kuwa mmeshinda. Watu wa Karatu hakikisheni mawakala wenu mnawapelekea maji na Chakula sababu mchana utakuwa mrefu.

Wanasema tukishinda hatutangazwa, tukishinda nasema tutatangazwa iwe kwa heri au shari. Wakigoma kututangaza wanataka shari na tutawapa shari.

Karatu mgombea ubunge Wenu ni *Cecilia Paereso* lakini pia hakikisheni madiwani wenu wanashinda kila kata ili CCM isipate hata diwani wa dawa, ikifika Saa 10 jioni sogeeni kwenye vituo vyakuhesabia Kura, kalindeni kura na tukishinda hakikisheni tunatangazwa.

Tarehe 28 mkajitokeze kwa wingi kupiga kura.

Ahsante Karatu na Mungu awabariki sana.
 

Attachments

  • IMG_6423.jpg
    IMG_6423.jpg
    176.8 KB · Views: 1
  • IMG_6389.jpg
    IMG_6389.jpg
    166.3 KB · Views: 1
  • IMG_6359.jpg
    IMG_6359.jpg
    237.3 KB · Views: 1
  • IMG_6367.jpg
    IMG_6367.jpg
    148.6 KB · Views: 1
  • IMG_6407.jpg
    IMG_6407.jpg
    260.1 KB · Views: 1
  • IMG_6402.jpg
    IMG_6402.jpg
    130.7 KB · Views: 1
  • IMG_6405.jpg
    IMG_6405.jpg
    146 KB · Views: 1
  • IMG_6376.jpg
    IMG_6376.jpg
    247.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom