Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda, ameendelea na ziara yake ya kuangalia jinsi huduma za uandikishaji wa wananchi wenye sifa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika Jumatano, Novemba 27, 2024, zinavyotolewa.
RC Makonda amefanya ukaguzi katika vituo zaidi ya saba ndani ya Wilaya ya Arusha, ambapo akiwa kwenye vituo hivyo, amesisitiza umuhimu wa kujiandikisha kwa kusema kuwa kama mtu hajajiandikisha hamna haja ya kulalamika iwapo viongozi watakaochaguliwa watakuwa ni wabovu.