Huyu mama aligoma kusaini matokeo akidai hasaini hadi Lowaasa aje hapo ktk ukumbi wa jiji la ARUSHA. Ni kweli wale jamaa pale walimsubiri, naye huyu fisadi wa Monduli akaja na akaingia ndani ya chumba cha mkutano wao. Akaja na hoja ya kutaka kura zirudiwe kuhesabiwa upya. kwa mujibu wa sheria, matokeo hayahesabiwi huku wanakohesabia sasa. Jamani hii inakuwaje? hebu nisaidieni mwenzenu mie siyo mtaalam wa sheria za uchaguzi. Inakuwaje mgombea wa jimbo lingine (Monduli) aje kuwa mshauri na hakimu wa jimbo lingine (Arusha mjini). Huu ni wizi.
HAKI HUINUA TAIFA!