Pre GE2025 Arusha Mjini: Mrisho gambo aahidi kugawa mitungi ya gesi kwa wazee 182

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
"Tunayo kampeni inayoendelea ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya masuala ya nishati safi ya kupikia, kampeni ambayo inakwendaa kuokoa mazingira yetu, na ambayo sisi kwenye mji wa utalii tunatakiwa tuipigie chapuo zaidi kwa sababu utalii na mazingira vinaendana. Makundi mengi yameshirikishwa, walemavu, akinamama, vijana na makundi mengine yote, tulikuwa tumebakiza kundi hili la wazee."

"Wazee wote hawa kila mmoja nyumbani kwake ana jiko la gesi, lakini tukasema ni vizuri baada ya kampeni hii unapokwenda mwalimu kufundisha ni lazima upewe kitendea kazi na kwenye masuala ya nishati safi kitendea kazi ni jiko la gesi la kupikia, kwahiyo tumeona leo baada ya kumaliza mazungumzo yetu ya leo tutaweza kutoa jiko la gesi kwa kila mzee ili anapokwenda kule nyumbani akatusaidie kutoa elimu. Kila kata watu saba jumlisha na viongozi kwenye ngazi ya wilaya tukapata idadi yao 182, tutahakikisha watu wote 182 majiko hayo ya gesi yanawafikia mpaka walipo."

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Gambo ameyasema hayo Arusha mjini kwenye hafla ya Uhamasishaji wa Kutoa Elimu ya Nishati Safi kwa Viongozi wa Baraza la Wazee Arusha.

Nishato safi Ipi? Arusha ukizunguka kote mjiji kumejaa majiko ya mkaa zunguka Baa zote ni migahawa yote ni majiko ya mkaa. Hizi ni hadaaa za j
kuhadaa wajinga wa hili Taifa.
 
"Tunayo kampeni inayoendelea ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya masuala ya nishati safi ya kupikia, kampeni ambayo inakwendaa kuokoa mazingira yetu, na ambayo sisi kwenye mji wa utalii tunatakiwa tuipigie chapuo zaidi kwa sababu utalii na mazingira vinaendana. Makundi mengi yameshirikishwa, walemavu, akinamama, vijana na makundi mengine yote, tulikuwa tumebakiza kundi hili la wazee."

"Wazee wote hawa kila mmoja nyumbani kwake ana jiko la gesi, lakini tukasema ni vizuri baada ya kampeni hii unapokwenda mwalimu kufundisha ni lazima upewe kitendea kazi na kwenye masuala ya nishati safi kitendea kazi ni jiko la gesi la kupikia, kwahiyo tumeona leo baada ya kumaliza mazungumzo yetu ya leo tutaweza kutoa jiko la gesi kwa kila mzee ili anapokwenda kule nyumbani akatusaidie kutoa elimu. Kila kata watu saba jumlisha na viongozi kwenye ngazi ya wilaya tukapata idadi yao 182, tutahakikisha watu wote 182 majiko hayo ya gesi yanawafikia mpaka walipo."

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Gambo ameyasema hayo Arusha mjini kwenye hafla ya Uhamasishaji wa Kutoa Elimu ya Nishati Safi kwa Viongozi wa Baraza la Wazee Arusha.

Mkuu hapo Dar tu kuni na mkaa basi ndio njshati kuu, sasa hapo ni jijini, saaa oiga picha mikoani huko, hizi hadaa wadanganye nazezeta wa hili Taifa.
 
Back
Top Bottom