Uchaguzi 2020 Arusha mjini: Queen Sendiga aendelea na kampeni za kiti cha Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Arusha mjini: Queen Sendiga aendelea na kampeni za kiti cha Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

ADC Party

Member
Joined
Sep 14, 2020
Posts
28
Reaction score
29
Tunachimba madini hapa na kuuza nje,pesa imayopatikana kwa wachimbaji na serikali sio kubwa Kama tungekua na kiwanda cha kuprocess madini hapa kwetu, nikipata nafasi ya kuongoza nchi hii serikali ya ADC itajenga kiwanda kikubwa ili kuongeza thamani ya madini yetu tuuze kwa Bei kubwa zaidi kiwanda kitatoa ajira kwa watanzania kipaumbele kikiwa ajira kwa wananchi wa Arusha.

Kwa mji mkubwa na wa maarufu Kama Arusha ufungwajwi maduka ya kubadilishia fedha ni msiba mzito, wengi wamekosa ajira na maisha yamedorora na serikali imekosa mapato pia, ADC ikipata ridhaa ya watanzania itakwenda kufungua maduka hayo ili kurudisha ajira na mapato, pia itaweka utaratibu wa kuhakikisha miamala yote inajulikana na serikali katika katika taratibu za kibenki.

Mgombea amesema hayo alipotembelea na kusalimia wananchi na wafanyabiashara maeneo mbalimbali mkoani Arusha na soko kubwa la Kilombero na soko kuu

Mgombea pia alisimama kusalimia wananchi wa mji mdogo wa Himo mkoa wa Kilimanjaro akiwa njiani kuendelea na kampeni zake mkoa wa Tanga wilaya ya Handeni kesho.

1442154127.jpg
2045738782.jpg
715942833.jpg
 
Huyu mama anahubiri amani sio km yule jamaa kutoka ubeligiji anaropoka matusi tu
 
Back
Top Bottom