Wanajukwaa habari za muda huu!
Anataka kuhamia Kagera(muleba) kutoka Arusha mjini.
Ni mfanyakazi wa serikali mambo ya mifugo na uvuvi, Yeye anaona akienda huko atapata fursa nyingi zaidi kulingana na kazi yake tofauti na hapa Arusha mjini.
Anataka akajiwekeze hasa kwenye ufugaji na uvuvi, je hapo muleba Kwa wenyeji panafaa?
Je fursa zingine za ziada ni zipi tofauti na yeye anazowaza? Nawasilisha karibuni Kwa ushauri.
Atasoma Kila ushauri maamuzi yatabaki kwake.