mbacho massawe
JF-Expert Member
- Apr 24, 2016
- 299
- 245
Wakati naishi Arusha, kuna kipindi nikawa nimesimamishwa kazi gHafla na sikuwa nimejipanga vizuri, kwa hiyo muda mwingi nilikuwa nafanya kazi ya kutafUta kazi nyingine wakati mwingine nakaa tu ndani kama furnitures.
Kwa wakati ule mwisho wa mwezi unafika sikuwa na pesa za kutosha za kulipa kodi ikabaki niwe nacheza michezo ya kuhide and seek na mwenye nyumba ili ku-avoid maswali mengi. Mwenye nyumba alikuwa anakuja hata saa tano usiku kugonga mlango adai kodi.
Nikapata idea, kuna jamaa fUlani alikuwa anasaka chumba na hana mahali pa kuishi na yuko karibu na hilo eneo, kwa hiyo nikamwambia nina geto naweza kustay na wewe Halafu tuwe tuna lipa kodi 50/50. Anatoa nusu natoa nusu.
Ilikuwa single room, kodi ilikuwa Tsh 30,000/= kwa kuwa jamaa alikuwa hajui na ilikuwa ni vigumu kupata chumba kwa haraka wakati ule akaona bora tukae pamoja.
Sheria zilikuwa simple, mwenye nyumba analala kwenye kitandani na mpangaji analala kwenye kochi kama cusion, kodi ananipa mimi kama internal landlord kisha mimi nampelekea external landlord. As simple as that. Msosi kila mtu anajitegemea .
Tukakaa miezi miwili jamaa akilipa kodi nzima. Maisha yalikuwa malaini sana hadi siku mpangaji wangu alipoanza kujuana na majirani halafu akagundua amekuwa akilipa kodi yote na si nusu. Mpangaji wangu akashikwa na hasira akahama.
Hapo bado maisha yalikuwa yana nichapa hatari, na bado nilikuwa sijapata kazi ya kueleweka ambayo naweza kujitegemea. Nilikuwa nimezoea ku-hustle pesa za chakula peke yake mwisho wa mwezi ulipofika nikarudia ule mchezo wa ku hide and seek huku nikijaribu kujazia pesa ya kodi.
Nikacheza deal na jirani wa pembeni yangu , ikifika usiku awe anakuja ananifungia kwa nje ili mwenye nyumba akija kubisha usiku adhani mwenye nyumba hayuko, then jirani anakuja kunifungulia asubuhi akienda kazini.
Kwa siku mbili mchongo ulienda poa, nilikuwa nasikia mwenye nyumba anagusa gusa kufuli halafu anavuta kwa nguvu najua niko salama kwa ajili ya usiku mwingine. Nilikuwa nimechanga 20000 na nilijua hawezi kuchukua pesa nusu hadi nijazie.
Halafu nilikuwa nimeshapata kazi nyingine ingawaje nisingeanza kupata pesa mapema.
Siku ya tatu tukafanya mchezo kama kawaida, church mouse nikachukua position kwenye bed nikausaka usingizi , mtoto wa watu sina tabu, kitu kama saa sita nikaskia mtu anagusa mlango nikajua ni mwenye nyumba.
Raia sikushtuka, nilijua niko salama nikalala kama maziwa yaliyoganda. Kwanza una deni la mtu lakini hawezi kukudai kwa kuwa hamuonani, mtu unalala zako kama maiti.
Asubuhi nikasikia jirani ana gonga mlango, nikaamka kama kawaida kumuuliza mambo ni gani, jamaa akaniuliza kama ni mimi nimeongeza kufuli la pili? Nikajua bhangi si mboga, nitajifungia vipi ndani ya nyumba na niko ndani?
Kumbe mwenye nyumba aliona kufuli langu liko lonely inapigwa na baridi pekee yake usiku mzima akaamua kuiongezea company, mlango wangu ukafungwa na kafuli mbili kama hardware. Jirani akaenda kazini kaniachia shida zangu.
Nikajua kitumbua kimeingia mchanga na siku za mwizi ni arobaini. Nipende nisipende nilijua ni lazima tu nimuambie mwenye nyumba niko ndani vinginevyo nitaozea ndani ya hiyo nyumba.
Halafu jambo moja baya zaidi choo kilikuwa nje ya nyumba, ni hizi nyumba zenye watoto wa kishua ambazo choo wanaita community toilets na nilikuwa nimebanwa hatari na hapo kuna mambo mawili nimuite mwenye nyumba tuongee au nikojoe kwenye jagi Niliamua kukojoa kwenye jagi.
Kufika mida kama saa sita nikajua ujinga hauna dawa kwa sababu ni lazima tu nitamuita mwenye nyumba, nikaanza kugonga mlango ili mtu aliyeko nje akiskia nimwambie amuite mwenye nyumba. Katoto ka jirani kakaskia nikakatuma kumuita mwenye nyumba. Swali la kwanza lilikuwa "Ulipitia wapi ukaingia ndani?"
Ikabidi ni mwambie nilikuwa ndani lakini kuna mtu alinifungia kwa njee, akasema ni yeye alifunga kwa nje lakini kulikuwa na kufuli ingine na halioni. Nikamuambia siwezi jua nilikuwa nimelala sana.
Akadai atatoa kufuli lake namlipa kodi yake vinginevyo nyumba yake si ya kukaa bure, nikampa 20000 nilikuwa nazo, nikampitishia chini ya mlango akachukua akasema "Jazia hizo zingine ndio nikufungulie" akasepa.
Ilibidi ni hustle nipate 10000 la haraka kwa mshikaji ndio huyo mzee akanifungulia. Then akanipa notice ya kuhama kwa kuwa namsumbua kulipa kodi. Sikuwa natamani kuhama hapo kwa sababu ile ndio ilikuwa nyumba yenye kodi ndogo.
Nikamtuma rafiki yangu aende amlipe jamaa pesa yake na ajifanye anataka nyumba. Mimi nae nikatafuta pickup inisaidie kuhama kisha nikamuambia huyo mzee wa pick up nina deal nataka tufanye, akasema haina noma bora natoboka pesa.
Siku ya kuhama tukaweka vitu kwenye pick up vizuri tukahama, tukapiga navyo raundi hapo town ni kama tuko road show ya wapangaji. Tulikuwa tunangoja mwenye nyumba amuonyeshe mwanangu geto kisha tukarudisha vitu kama mpangaji mpya[emoji41].
So kazi zili-change, best yangu ndio alikuwa landlord wangu, nilikuwa nampelekea kodi then yeye anampelekea mwenye nyumba.
Niligundua kodi ni muhimu sana kwa jiji kama Arusha. Ukilipa on time unaweza hata kukaa kwenye nyumba ya mwenye nyumba huku umeweka miguu juu ya meza umtume jikoni

Upvote
2