Arusha: Njia za watembea kwa miguu walikohamishwa wamachinga, zageuzwa maegesho ya magari

Arusha: Njia za watembea kwa miguu walikohamishwa wamachinga, zageuzwa maegesho ya magari

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,325
Reaction score
2,491
Habari wadau,

Zoezi la kuhamisha wamachinga waliokuwa wameziba njia za watembea kwa miguu lilifanyika kwa malengo mengi ikiwa ni pamoja na watembea kwa miguu kupata njia za kupita. Wenye magari nao walikuwa walalamikaji wakubwa juu ya kero hiyo ya wamachinga kuziba barabara.

Baada ya zoezi la kuwaondoa wamachinga kwenye njia za waenda kwa miguu, njia hizo zimegeuzwa sehemu za kuegesha magari kama inavyoonekana kwenye picha.

Hili ni kwa hapa Arusha sijui mikoa mingine kama DSM na Mwanza. Tuseme hii nchi Sasa kila mmoja anajifanyia anavyotaka, hakuna Sheria ama mtu akiona fursa anaitumia kikamilifu. Nafikiri malmaka husika zilifanyie kazi jambo hili.
#hakiza#watembea#kwamiguu#

IMG_20211208_112649_049.jpg
 
Zanzibar wamachinga wanafanya biashara zao kwa uhuru mkubwa wamepewa na vitambulisho.
Haa haa just haa haa machotala na mahisibula sio… umesahau Mwanza waliachwa wafanye biashara wazanzibari wakapelekewa majeshi na kupigwa risasi. Kutesa kwa zamu.
Mama na Magufuli ni kitu kimoja ..na kwa ukabila na ubaguzi wa rangi pia, wewe ulifikiri roho ya ubaguzi wa Samia itaishia kuwafunga kina MBOWE. Poleeee..
Njooni tudai katiba mpya pamoja ndio dawa ya maujinga yote haya.
 
Zanzibar wamachinga wanafanya biashara zao kwa uhuru mkubwa wamepewa na vitambulisho.

Huku bara wanafukuza wapiga kura na kutetea yasiyo piga kura.

Tangu lini mwenye gari na biashara zake akaenda kushinda kwenye foleni akichomwa na jua ili apige kura?
Kupiga kura sio sababu ya kuvunja sheria
 
Kumbe Arusha ni jina tu. Ni pabaya tu kama miji mingine
 
Zanzibar wamachinga wanafanya biashara zao kwa uhuru mkubwa wamepewa na vitambulisho.

Huku bara wanafukuza wapiga kura na kutetea yasiyo piga kura.

Tangu lini mwenye gari na biashara zake akaenda kushinda kwenye foleni akichomwa na jua ili apige kura?
Kodi yao ndiyo inaendesha nchi, kura ibeni kama kawaida yenu
 
Back
Top Bottom