Arusha: OC CID atinga kizimbani kutoa ushahidi kesi ya Ole Sabaya

Arusha: OC CID atinga kizimbani kutoa ushahidi kesi ya Ole Sabaya

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
Baada ya kuahirishwa Jana kesi ya Unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Sabaya na wenzake ,kesi.hiyo imeendelea Leo Kwa mkuu wa polisi wa wilaya ya Arusha (OC CID) ASP Gwakisa Minga (45)ambaye ni shahidi wa Saba kutoa ushahidi wake.

Sabaya alitinga mahakamani hapo majira ya asubuhi chini ya ulinzi mkali wa askari magereza, akiwa na Kaunda suti ya bluu huku mkono wa kushoto akiwa na plasta ya Dripu inaloashiria kuwa alikuwa ametundikiwa chupa ya Dripu.

katika kesi hiyo namba 105 ya mwaka.huu Gwakisa ameieleza mahakama jinsi alivyompokea kituoni mlalamikaji Bakari Msangi akiwa kwenye hali mbaya ya kipigo kizito akiwa anavuja damu masikioni.

Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Minga ambaye ni mrakibu wa jeshi la polisi alisema kuwa alimpokea Bakari Msangi February 10 mwaka huu saa sita usiku katika kituo Cha polisi akiwa na majeraha makubwa ya kipigo usoni huku damu zikimtoka masikioni.

Alidai kuwa siku ya Februari 9 mwaka huu majira ya saa sita siku alipigiwa simu na mkuu wa polisi wa wilaya ,OCD Mchunguzi akimtaka afike kituo Cha polisi haraka kwani diwani wa Sombetini Bakari Msangi alikuwa amepigwa na kuporwa.

Shahidi alidai kuwa Taarifa hiyo ilimlazimu kuwapiga simu askari wake Sajenti Onuku na Koplo Called na kuwataka wawepo kituoni hapo kwa ajili ya kuchukua maelezo ya mlalamikaji .

Alidai walimhoji Msangi kuhusu alama za kipigo usoni ,ambapo aliieleza kuwa Sabaya na vijana wake walimpiga na kumpora fedha tasilimu kiasi cha sh,390,000 .Pia alieleza kuwa wamteka na kumzungusha maeneo mbalimbali katiika jiji la Arusha na baadaye katika hotel ya Tulia iliyopo Mianzini.

Shahidi alidai kuwa alimwagiza Sajenti Onuku kuchukua maelezo ya Msangi na baadaye alimpatie fomu namba tatu ya polisi (PF3)Kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Alieleza kwamba baada ya kuandikwa maelezo kituo Cha polisi Msangi alipatiwa PF3 ambapo shahidi aliongozana naye hadi katika hospital ya Mkoa Mount Meru ambapo Msangi akitibiwa na baadaye daktari alijaza PF3.

Shahidi alidai kuwa baadaye alikabidhiwa PF3 na kuitunza eneo salama na baada ya kukamilika kwa uchunguzi aliambatanisha PF3 kwenye jalada la mlalamikaji na kulipeleka Kwa mwanasheria wa serikali.

Wakili Mwandamizi wa serikali Abdalah Chavula alimtaka Shahidi huyo kuitambua PF3 mahakamani ,ambapo shahidi aliitambua kuwa ni Mali ya jeshi la polisi na kuiomba mahakama iipokee kama kielelezo,ambapo kilipokelewa kama kielelezo namba moja.

Shahidi alidai kwamba February 12 mwaka.huu majira ya saa 10 aliongoza kikosi Cha askari wa upelelezi kwenda eneo la tukio katika duka la Shaahid Store lililokuwa limefungwa tangu siku ya tukio Februari 9 mwaka huu.

Alidai kuwa akiwa ameambatana pia na Norman Jasim muuzaji wa duka hilo alifungua duka nankuingia ndani ambapo walikuta baadhi ya bidhaa zikiwa zimevurugika huku chini ya sakafu kukiwa na matone ya damu na Maji.

Shahidi aliieleza kuwa Camera nne za CCTV zinazotumika katika duka hilo zilikuwa zimechezewa na kugeuziwa ukutani huku kamera mbilizilizobaki hazikuweza kurekodi tukio vizuri.

Alidai kuwa muuzaji wa duka hilo Norman Jasim alikagua vizuri na kugundua kuwa ndani ya duka hilo mashine mbili za EFDs pamoja na fedha za mauzo zilichukuliwa .

IMG_20210805_091805_796.jpg
 
Kuna video iliwahi kua posted online ikionyesha mtu akiwa anapigwa ndani ya duka na ikasemwa ni Sabaya akiwa anampiga muuza duka.

Huku uswahilini kwetu ukienda polisi kuripoti juu ya tukio la kupigwa na ukamtaja mhusika askari ataenda kumkamata mhusika. Kama diwani alimtaja Sabaya lakini mpaka wanaenda dukani nafikiri Sabaya hakua amekamatwa.

Walienda kufanya nini dukani? Kuchezea cctv
 
Hii kesi naiona ngumu kwa sabaya lakini cha ajabu namuona hana stress kabisa yani
 
Sabaya kesi imemkalia vibaya, naona wanaitoa live ili hakimu akose pakumchomoa .
 
Sabaya kesi imemkalia vibaya, naona wanaitoa live ili hakimu akose pakumchomoa .
Wanamtoa live wenyewe ili isionekane kaonewa ndio maana hakimu katolewa mkoa mwingine kabisa kuja kumaliza kesi za Arusha siku 14 mfululizo aende tena huko Moshi kwenye kesi zake zingine huyu Moshi ataenda akiwa na jezi tayari labda waruke hukumu...
 
Polis ikijisimamia yenyewe n jesh linalokua na uelekeo mzuri wa kutenda haki bila kuangalia nani kafanya kosa gani
Tatizo linakuja pale maCCM yanapojidai hii nchi ni yao yan mkuu wa wilaya anaweza kukuweka lockup masaa 24 hata bila kosa lolote na kesho akasema utolewe eti wanaita lockup kwa amri ya mkuu wa wilaya/mkoa
 
Kuna video iliwahi kua posted online ikionyesha mtu akiwa anapigwa ndani ya duka na ikasemwa ni Sabaya akiwa anampiga muuza duka.

Huku uswahilini kwetu ukienda polisi kuripoti juu ya tukio la kupigwa na ukamtaja mhusika askari ataenda kumkamata mhusika. Kama diwani alimtaja Sabaya lakini mpaka wanaenda dukani nafikiri Sabaya hakua amekamatwa.

Walienda kufanya nini dukani? Kuchezea cctv
Kucheza kombolela.
 
Back
Top Bottom