Arusha: OC CID atinga kizimbani kutoa ushahidi kesi ya Ole Sabaya

Sabaya kesi imemkalia vibaya, naona wanaitoa live ili hakimu akose pakumchomoa .
Hakimu wa kesi hii wamemtoa Geita maalum kwa hio kesi, nadhani baada ya kuona wa hapo Arusha wameshatembezewa 'mpunga' wa kutosha.
 
Wanamtoa live wenyewe ili isionekane kaonewa ndio maana hakimu katolewa mkoa mwingine kabisa kuja kumaliza kesi za Arusha siku 14 mfululizo aende tena huko Moshi kwenye kesi zake zingine huyu Moshi ataenda akiwa na jezi tayari labda waruke hukumu...
Mkuu sijaelewa Moshi akiwa na jezi zipi? Iweke vzr sijakusoma
 
Shahidi wa saba wa Jamhuri, ASP Gwakisa Minga anaendelea kutoa ushahidi wake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo(Sabaya), kufika mahakamani.

Minga ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Arusha alianza kuongozwa juzi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula.

Jana kesi hiyo ilishindwa kuendelea kusikilizwa kufuatia mshitakiwa huyo kushindwa kufika mahakamani kutokana na kuumwa.

Leo Alhamisi Agosti 5, 2021 Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo, Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura waliwasili mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi kwa ajili ya kuendelea na shauri hilo lililoanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Septemba 19, 2021.

Soma zaidi hapa: Upelelezi Kesi ya uhujumu uchumi ya Sabaya bado, ya unyang'anyi wa kutumia silaha yaendelea

Mshitikiwa huyo alipoulizwa na hakimu huyo kuhusu maendeleo ya afya yake aliieleza mahakama kuwa anaendelea vizuri na anaweza kufuatilia mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ya jinai namba 105, 2021.

Chanzo: Mwananchi

My Take:
Juzi nimesikiliza maelezo ya Mrakibu Msaidizi wa Polisi Gwakisa Minga ambaye ni Mkuu wa Upepelelezi na ni shahisidi wa upande wa mashataka kwenye kesi hii. Nachelea kusema kambi ya utetezi ya DC mstaafu ina hali mbaya. Jahazi linazama, na maswahiba wanamkataa!
 
Umesema Shauri hilo limeanza kuskilizwa September? Au Kilimanjaro mbili nilizopiga hapa zinanivuruga?
 
Niliandika hapa kuwa kesi imelemea Sana kwa sabaya labda Hakimu ajitoe ufahamu kupita kiasi
 

Sikuwahi kujua huyu Dogo ni mpumbavu wa kiwango hiki.... watu wana tafuta fedha kwa shida wewe uibe tu kirahisi.
 

Inaonekana unaishi Rwanda, ya huku yaache hayakuhusu, Kama kule kawe wakati wa uchaguzi kulikuwa na ma bag ya kura Feki, Hii kesi iliishia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…