Arusha: Rushwa yadaiwa kutawala tajiri wa Madini aliyeua mlinzi aachiwa huru

Arusha: Rushwa yadaiwa kutawala tajiri wa Madini aliyeua mlinzi aachiwa huru

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Mfanyabiashra wa madini mkoani Arusha, Pendael Moller ameondolewa kwenye kesi ya mauaji ya mlinzi anayefahamika kwa jina la Steven Jimmy na kuwaacha wenzake wawili ambao ni onesmo Molleli na Deogratius Mollel.

Mwanasheria wa Serikali alimwambia Hakimu Devota Msofe kuwa serikali imeamua kumwondolea shtaka mshtakiwa wa tatu Pendael Mollel katika kesi ya mauaji ya mlinzi wa nyumba ya Mahamud Mohamed yaliyofanyika Aprili 20, 2022.

Baada ya kuwasilishwa kwa pendekezo hilo na mwanasheria wa serikali Janeth Mason, Hakimu Devota Msofe alimwachia huru mshtakiwa huyo na wengine wawili wataendelea kukaa rumande hadi kesi yao itakapotajwa tena Juni 9, 2022.

Baada ya kuachiwa huru kwa mfanyabiasha huyo familia ya marehemu imesema haijakubaliana na suala hilo kwani inavyoonekana kuna baadhi ya matapeli wanaojifanya ndugu wamehongwa pesa na kwamba watakutana kama ndugu na kutoa tamko.

Awali, kabla ya kesi kupelekwa Mahakamani ndugu wa marehemu walizungumza na vyombo vya habari walisema kuwa mfanyabiasha huyo Pendael ndie aliyekuja kumchukua marehemu kazini kwake na kuondoka nae na baadaye kupata taarifa za kifo chake.

mlinzi aliyeuliwa
 

Attachments

  • 20220423_215123.jpg
    20220423_215123.jpg
    46.1 KB · Views: 21
Tayari ndugu washazungukana,wamepita mlango wa nyuma wakalamba minoti kwa ushiriakno wa Polisi...
 
Tajiri hafungwi,nenda kule Tarime uone mauaji yanavyofanywa na hawa matajiri na hakuna aliyefungwa, yaani huwa wanashindana kuua lakini hakuna anaefungwa.
 
Ukiwa tajiri kwenye nchi za ulimwengu wa tatu unakuwa juu ya sheria
 
Tajiri hafungwi,nenda kule Tarime uone mauaji yanavyofanywa na hawa matajiri na hakuna aliyefungwa, yaani huwa wanashindana kuua lakini hakuna anaefungwa.
Umenikumbusha Kisire mdogo alivyochomoka Boman pale
 
Back
Top Bottom