Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, Mkoa wa Arusha, wagombea tisa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameondolewa kwenye mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wagombea hao kukosa sifa zinazotakiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi, wagombea hao wameenguliwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo mitaa wanayogombea kutokuwa kwenye orodha rasmi ya mitaa inayotambulika na Mamlaka ya Serikali za Mitaa, pamoja na baadhi yao kushindwa kutaja jinsia kwenye fomu walizojaza.
Soma pia: CHADEMA: Baada ya Waziri wa TAMISEMI kusema Wagombea walioenguliwa wakate rufaa, tumepokea taarifa ofisi za Mitaa, Vitongoji na Vijiji zimefungwa
Wagombea walioathirika na hatua hii ni pamoja na Frank Samwel Laizer aliyekuwa akiwania uenyekiti wa Mtaa wa Mbeshere, David Molel aliyekuwa akigombea uenyekiti wa Mtaa wa Olkungu, Mohamed Amir aliyekuwa na ndoto za kuongoza Mtaa wa Makaburi ya Baniani, na Juma Waziri aliyekuwa akigombea uenyekiti wa Mtaa wa Mkwangwaru B.
Pia, kuna wagombea wa nafasi ya ujumbe wa Serikali za Mitaa, kama Hayrat Manyanga na Gilbert Massawe, ambao nao wameondolewa kwenye mchakato huu baada ya kukosea kwenye ujazaji wa fomu zao za kuwania nafasi hizo.