Pre GE2025 Arusha: Wajumbe wa CCM wamkataa Katibu wa chama hicho kwenye Wilaya ya Monduli kisa kupanga safu ya watakaogombea Ubunge 2025

Pre GE2025 Arusha: Wajumbe wa CCM wamkataa Katibu wa chama hicho kwenye Wilaya ya Monduli kisa kupanga safu ya watakaogombea Ubunge 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wameungana kumkataa Katibu wa Wilaya wa Chama hicho Rukia Omary kwa kile walichokidai kuwa kiongozi huyo amekua akikiuka kanuni za chama ikiwemo uchonganishi wa Viongozi pamoja na upangaji safu ya watao gombea Ubunge 2025.



Kufuatia hali hiyo ManaraTv imemtafuta Katibu huyo wa CCM Rukia Omary kutaka kujua ukweli wa tuhuma zinazotolewa na Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.

Soma pia: Fred Lowassa achukua fomu ya kuomba ubunge Monduli kupitia CCM

Katika mazungumzo yake Katibu huyo ameelezea kuwa tuhuma hizo zilianza tangu uchaguzi wa Serikali za mitaa na kinachoendelea ni mbinu za uchonganishi ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya watu ndani ya CCM wenye uchu wa madaraka ambao wamekuwa wakipiga kampeni za wazi kwa nia ya kugombea Ubunge.
 
Back
Top Bottom