Arusha: Wanahisa wamfagilia Mkurugenzi wa CRDB Dk. Charles Kimei, waomba aongezewe mkataba

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa Benki ya CRDB unaofanyika leo Mei 19, 2018 jijini hapa, wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk Charles Kimei kuendelea kuitumikia benki hiyo.

Kauli za wanahisa hao waliohudhuria mkutano mkuu wa 23 wameeleza hayo baada ya Dk Kimei kuwajulisha kuwa kwenye mkutano mkuu ujao, atawaaga rasmi.
"Hotuba yangu ya leo si ya mwisho. Tutakutana tena mwakani nitakapowaaga. Mkataba wangu unaisha Mei, 2019,” amesema Dk Kimei alipokuwa akitoa hotuba ya mwenendo wa benki hiyo ambayo mwaka 2017 imepata faida ya Sh36 bilioni ambayo imepungua kutoka Sh70 bilioni iliyopata mwaka 2016.

Kwenye michango yao, baadhi ya wanahisa hao wamesema kipindi hiki ni kigumu kiuchumi hivyo CRDB inahitaji mtu mwenye uzoefu wa kutosha kukabiliana na changamoto zilizopo.

Mmoja wa wanahisa hao, Lemburis Sirikwa (76) wa Arusha amesema endapo mkurugenzi huyo ataondoka na kuiacha benki hiyo, ndani ya miaka miwili ya kutokuwa naye lazima ufanisi utapungua.
"Kimei shall remain until further notice (aendelee kuwepo mpaka taarifa nyingine itakapotolewa).

Kama bodi haitaki kufanya hivyo, tutachagua wajumbe wengine," amesema Sirikwa.
Siri kwa amesema wapo wakurugenzi wenye umri wa miaka 90 lakini wanaendelea kuziongoza taasisi zao hivyo haoni sababu ya Kimei kustaafu.

"Kimei ni mdogo sana. Mimi nina miaka 76, namzidi mbali sana. Asiondoke sasa hivi," amesema.
Mwanahisa mwingine kutoka mjini Sumbawanga, Kapteni mstaafu Noel Nkoswe amesema suala la kumpata mkurugenzi ni gumu.

"Tulipoanza, tulitafuta mtu anayefaa lakini hatukupata. Mwishowe tukaenda kuiomba Benki Kuu ambayo ilitupatia Dk Kimei. Tunaishukuru Benki Kuu kwa kutupa mtaalamu huyu, napendekeza aendelee kuwepo walau miaka miwili au mitatu zaidi," amesema.
 
Kimei anafaa kurithi mikoba ya Dr Mpango
 
Ila chonde chonde wasije sema kuwa Dr. ..naye ni chaguo la aliyejuu ya mbingu.
 
Tuwaheshimu wanahisa na maoni yao please. Sisi waweka pesa tuwe na subila sw
 
Apumzikie zake huko!! Benki kila mwaka faida inshuka kutokana na sababu za 'hovyo' - mikopo mfu.
 
Je gawio kwa mwaka huu in shilingi ngapi kwa hisa?
 
Wanahisa wa bank ya CRDB wamemwagia sifa mkurugenzi mtendaji wa bank hiyo Dr Charles kimei kutokana na uongoz wake uliotukuka ambapo bank hiyo ni bank ya kwanza kwa ubora Africa Mashariki

Wakizungumza ktk mkutano wa kukabidhi ripoti ya utendaji, wamesema kwakuwa Dr kimei atastaafu mwakani wao wanasikitika sana wakihofu kuwa bank hiyo inaweza kuyumba ambapo wamekataa Dr kimei kustaafu

Licha ya Rais Magufuli kumuahidi Dr Kimei kuwa atampa kazi akistaafu CRDB, wanahisa hao wameazimia kumuongeza mkataba wa miaka 3 kwakuwa wao ndio wenye bank.

Dr Kimei alishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi huku akishukuru watu wote walioshirikiana nae kuipaisha bank hiyo kiuchumi.

Dr Kimei ambaye atatimiza miaka 60 mwakani, amezaliwa eneo la Marangu halmashauri ya wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro
 
ameibeba sana... kiukweli ameitoa mbali... lakini sio sababu ya kumlilia sababu kama akiumwa au akifariki itakuwaje... taasisi iwekewe misingi mizuri ambapo atakayekuja nae afanye yake
 
Kiongozi bora ni yule anaeombwa kuongoza na si yule anayelazimisha apewe nafasi ya kuongoza.... Hongera Dk. Kimei wanahisa CRDB wameona mchango wako na wameudhamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…