Sema tu kinacholeta maudhi, hao Iron Boys huwa wanabarikiwa sana kipaji cha ushawishi kwenye jamii kiasi cha kujikuta wanaaminiwa na hivyo kukabidhiwa majukumu makubwa, na yaliyo juu ya uwezo wao.
Golden Boys ukiondoa akili na maarifa mengi waliyojaliwa kichwani; bado wamenyimwa ule ujasiri wa kuchangamana na jamii, kujenga ushawishi, na pia kujitoa ufahamu. Ndiyo maana wengi wanaishia tu kulalamikia pembeni, kujinyamazia kimya, kupuuza, au hata kujitoa kabisa! Na hivyo kuacha mambo yajirndee tu yenyewe.. So sad for that. 🙁