KWELI Asali haiharibiki iwapo ikitunzwa vizuri hukaa Kwa miaka mingi

KWELI Asali haiharibiki iwapo ikitunzwa vizuri hukaa Kwa miaka mingi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimekuwa nikisikia na kusoma machapisho ya watu kuwa asali haihairbiki kabisa, je ni kweli? Na kwa ninihaiharibiki?

1733132337902.png
 
Tunachokijua
Asali hutengenezwa na nyuki, hutokana na mkusanyiko wa vimiminika vyenye sukari nyingi itokayo kwenye mimea ya Maua, Asali ina ladha ya utamu. Huhifadhiwa katika sega la asali ili kutoa chakula kwa nyuki. Kumekuwa na madai kuwa Asali haiwezi kuharibi hata ikikaa kwa miongo kadhaa ya miaka.

Je, ni upi uhalisa wake?

Jamiicheck imepitia Tafiti na Machapisho mbalimbali na kubaini kuwa ni kweli Asali huweza kukaa kwa muda mrefu wa miongo kadhaa iwapo itahifadhiwa vizuri kwa kufunikwa vizuri na kuwekwa eneo lisilo na unyevu unyevu.

Kwa mujibu wa Helthline asali ina kiwango kikubwa cha sukari(utamu) na kiwango kidogo cha unyevu, hii inaifanya asali kuweza kudumu kwa muda mrefu iwapo ikihifadhiwa vizuri.

Aidha, MDPI wanabaisha kuwa Asali ni hygroscopic, asali ina kiwango cha chini sana cha maji. Nyuki wanahusika na kukausha unyevu wa nektari iliyokusanywa, ambayo kwa kawaida huwa na unyevu wa 80-90%, na kuibadilisha kuwa asali nzito. Asali iliyokomaa hufikia tu unyevu wa asilimia 18.

Bila maji, bakteria hawawezi kuonekana wala kustawi. Asali iliyokomaa vizuri kwenye mzinga au kwenye chombo kilichofungwa ni salama dhidi ya bakteria.

Asali inaundwa zaidi na sukari, hii huzuia ukuaji wa vijidudu kutokana na changamoto za mgandamizo mkubwa wa osmolariti ndani ya asali.

PH ya asali ni asidi na ipo kati ya 2 na 4.5. Bakteria wengi hatari hupendelea mazingira ya pH ya kati au yenye alikali, hivyo hawawezi kukua wala kustawi katika mazingira ya asidi kama asali.

Vilevile, Katika mchakato wa kutengeneza asali, nyuki hutoa aina mbalimbali za enzyme, Mojawapo ni glucose oxidase, ambayo hutoa hydrogen peroxide, kemikali yenye uwezo mkubwa wa kuua vijidudu na kuzuia ukuaji wa vijidudu.

Mountain-Valley-Honey-Can-Honey-Go-Bad-4.jpg

Kwa upande wa Live Science Wanaeleza kuwa Muundo wa asali hutegemea na aina ya nyuki," Kantha Shelke, mwanasayansi wa chakula katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins na mwanzilishi wa Corvus Blue LLC, kampuni ya utafiti wa sayansi ya chakula na lishe iliyoko Chicago, aliiambia Live Science kuwa

Baada ya kukusanya nectar kutoka kwenye maua, nyuki hugeuza sucrose, mchanganyiko tata wa glucose na fructose, kuwa sukari rahisi yenye utamu sana. Ingawa asali mara nyingi ni sukari, pia ina zaidi ya dazeni ya vitu vingine, kama vile vimeng'enya, madini, vitamini na asidi za kikaboni. Asali pia ina flavonoid na phenolic, ambayo inajulikana kuwa anti-inflammatory na antioxidants, Wingi wa kemikali ambazo huungana wakati nyuki anatengeneza asali hufanya asili isiharibiwe na vijidudu ambavyo kwa kawaida huharibu chakula.
Nimekuwa nikisikia na kusoma machapisho ya watu kuwa asali haihairbiki kabisa, je ni kweli? Na kwa ninihaiharibiki?

Ni kweli. Kutokuharibika kwa asali lakini inategemea jinsi uhifadhi sahihi unavyozingatiwa.
Asali haiharibiki kutokana na uwepo wa vitu (chemical componds) ambavyo haviruhusu kustawi kwa bacteria au ukungu(fungus).
 
Asali ya nyuki au asali papuchi?
Kwa maana ya kipochi manyoya?
 
Back
Top Bottom